Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Hawatamki ndoa ila niruksa kuachwa fasta.
 
Tumalize mjadala wakuu nilienda kumuona ilikuwa jumamosi tukayamaliza
 
1. Kwa mujibu wa hili hadithi hii imeruhusiwa;-

In Madeenah there was a woman who circumcised women and the Prophet (peace and blessings of Allaah be upon him) said to her: “Do not go to the extreme in cutting; that is better for the woman and more liked by the husband.” Narrated by Abu Dawood (5271), classed as saheeh by Shaykh al-Albaani in Saheeh Abi Dawood.

Unaielezeaje?

2. Pili Circumcision kwa ujumla haipo kwenye Quran. Inasemwa Ni sunnah.

Nini maana ya Sunnah?
 
Mkuu kama unajua kingereza,hii habari uliyoieleza,umejijibu mwenyewe,ukweli hii hadith siijui,wala hamna katika Uislam sehemu yoyote iliyoeleza kumkeketea mwanamke ni sunna,..

maana ya sunna ni kufuata vitendo alivyofanya Mtume Mohamad kama Mtume amesema:-

"Do not go to the extreme in cutting; that is better for the woman and more liked by the husband" tafsiri = "Msifanye mambo yaliyokithiri(kupita mipaka) kwani hicho mnacho kikeketa ni kitu bora kwa mwanamke na zaidi kwa mume" --

kwa kiswahili cha kwaida msimkekete mwanamke kwani hicho mnachokikeketa ni bora kwake na ni bora kwa mumewe..

Hicho kitendo cha kukukeketa wanawake hakiwezi kuwa sunnah kwani tayari Mtume ameshakipinga,sunnah ni vitendo alivyofanya Mtume,Je Mtume Muhamad aliwakeketa wake zake!!?

Haina haja ya kuelezea ni watu gani wanakeketa wanawake zao,kwanini wanawakeketa,na kwanini uislam hauhusiani na hicho kitendo kwani nimeshaeeleza kwenye "comments" nyengine
 
Jamani mtueleweshe wenye imani ambazo mambo ya kutahiri, kukeketa hayafungamani na matendo mema ya kukupeleka mbinguni. Ni maswala ya kiafya km uambiwe kuchemsha maji ya kunywa kujikinga na maradhi lakini haihusiani na mambo ya kuuona ufalme wa Mungu! Rafiki yangu mmoja wakati akinihubiria imani yake na kwamba nisile kitimoto nilimhoji sababu zake akajikita kuzungumzia issues za afya. Huyu ni msomi, kwa hiyo nikamwomba aniorodheshee nchi kuhusu death rates na sababu zinazopelekea vifo hivyo. Kwa kifupi akajikuta nchi ambazo kitimoto ni one of their stapple food ndiyo zenye raia wenye afya tele na nchi zinazoamini kitimoto haifai vifo viko juuuuu! Msabato mmoja rafiki yangu Mzambia tukiwa naye masomoni Ng'ambo alikuwa hali kuku (wa kizungu) kwamba kulingana na mafundisho ya dini yao kuku hawa wana madhara makubwa kiafya (nakubaliana na hoja hii) lakini wakati huohuo alikuwa akikaanga mayai ya kuku walewale. Nilipomwuliza kuhusu sababu za kukataa kuku wakati huohuo anakula mayai yao akashindwa kujibu. Haya ndiyo mambo ya mtu kukaririshwa vitu na kuvikubali bila reasoning ya kutosha! Tatizo hili linawakabili hasa waislam kukaririshwa vitu bila kupembua ukweli! Ndiyo maana unakuta mwislam amekaririshwa tangu utotoni kuwa Yesu ni Mtume wa Mungu wakati huohuo hawafuati mafundisho ya wanayemwamini kuwa naye ni mmoja wa Mitume. Mtu anakaririshwa utume wa Yesu bila kuhoji inakuwaje awe Mtume halafu mafundisho yake hayafuatwi? Mkristo mwenye uerevu anakuja na conclusion kwamba Issa anayehubiriwa na waislam siyo Yesu anayehubiriwa na Wakristo. Wakristo imani two hawaendeshwi na mihemuko. Wanaendeshwa na facts, FULL STOP!
 
Yesu ni njia na kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila.....angali kuna roho inakufuatilia,kama wazazi wamekukatalia wasilikilize wazazi.
Kubadili Dini kwa ajili ya MKE au mume ni unafiki sijui ni wapi kwenye biblia wameandika kwamba wanafiki hawatoonja mbingu !
 
Badilisha uone cha moto ndiyo nishakwambia hivyo. [emoji23]
 
Sio lazima ubadili.
Wengi tu wanaishi na dini mbili.

Chaguo la mwisho ni lako.
Usifanye kitu kufurahisha watu fanya kitu kinachokufurahisha wewe.
 
Actually kitimoto ni nyama inayoliwa na watu wengi zaidi duniani. Kuliko aina yoyote ya Nyama.
 
Neno 'Sunnah' ina maana gani? Na neno Mutahab ina maanisha nini?
 
Mkuu kuhusu Kiti moto,sio Waislam tu ndio hawali Nguruwe,Wayahudi hawali Nguruwe vile vile,Yesu alikuwa Myahudi, Katika vitabu vya biblia na Kuran vyote vimekataza ulaji wa Nguruwe kwa binadamu,..

kama mwislam nilikuwa napata tabu sana kujua kwanini Kurani imekataza waisalam wasile Nguruwe,lakini baada ya kusoma Biblia ndio nikafahamu kwanini wanadamu wamekatazwa na Mungu wasile Nguruwe,katika agano la kale ukisoma
Walawi 11-7 imeandikwa:"Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi.".

Dini ya kiisalam na ya Kikristo ni muendelezo ya mafundisho ya kitabu cha Musa(Taurati=Agano la kale),Mafundisho ya taurati yanasema binaadamu ameruhusiwa kula wanyama wote wenye kwako isipokuwa Nguruwe,..

Mafundisho ya Bibile yanasema kuwa Nguruwe hasagi chakula tumboni,kwahiyo ukila nguruwe ni sawa na kula mzoga(najisi)

Kisayansi mfumo wa ndani wa umbo la nguruwe(Anatomy)ni ni sawa mwanadamu,yaani viungo vya ndani ya Nguruwe kama Moyo,maini,figo ni sawa na vya binadamu,kwa maana hiyo ukila Nguruwe ni sawa na kula binadamu..

Nchi za Ulaya takribani zote watu wanakula kiti moto,kuna baadhi ya madhehebu ya dini ya kikristo yameanza kukemea ulaji wa Nguruwe,Nguruwe wa ulaya wanadungwa sana shindano za antibiotic hili nalo ni tatizo kwa binadamu,kwani ukiwa mlaji sana wa nyama ya nguruwe, mwili wa mwanadamu mwisho unakuwa sugu unakuwa hautibiki kwa antibiotic

Kweli mkuu,waislam wanafundishwa tangu wadogo kuwa Yesu si Mungu ni Mtume wa Mungu kama alivyokuwa Musa,Daudi,Suleman na wengine,waislam wanafundishwa kuwa Yesu aka ISA aka ISO aka YOSHUA ni Masaya alikekuja kwa Wayahudi tu.,na Biblia inasema hivyo hivyo kama wanavyofundishwa waislam

Ukisooma Biblia kuanzia Matayo 15:22-24 utakuta kuna kisa cha mama ambae alimkimbilia Yesu akamuomba amtibu Yesu alikataa kumtibu kwasababu alikuwa sio Myahudi!!,wanafunzi wake walipigwa na mshangao,walipomuuliza Yesu kwanini kakataa kumtibu yule mama..

Matayo 15-24 "Yesu akajibu, “Sikutumwa ila kwa watu wa Israeli waliopotea kama kondoo tu.” kwa kiswahili cha kawaida "Nimetumwa kwa wayahudi wasio mcha Mungu tu,sio watu wengine"...mimi na wewe mkuu hatumo kwa mujibu wa Yesu mwenyewe


Mkuu ukisema waislam wanahemkwa hawafati "Facts" hawafati mafundisho ya yesu sio kweli,waislam wanamfata Yesu kivitendo,sio katika majukwaani,..

Yesu alikuwa Myahudi,wayahudi hawali Nguruwe,Waislam hawali Nguruwe,waislam wanakata Govi(kutahiriwa)Yesu alikatwa govi (Kutahiriwa) siku nane baada ya kuzaliwa,na mambo mengine mengi..Je wewe unayafanya haya??!

Luka2:21 "
Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba" ..

Kuna mistari mingi tu kwenye Biblia ambayo inadhihirisha kuwa Yesu ni mtume kama mitume mengine vile vile Yesu sio Mungu,Luka 2.21 ni mmoja wao,..

Mkuu unatakuwa ufanye utafiti usome historia ya ukristo ujue kwanini imefikia sehemu wakristo wengine wanamini kuwa Yesu ni Mungu wengine wanamini ni mtoto wa Mungu,wanapingana,katika dhehebu la kikiristo ambalo nimeona halina mhemko ni dhehebu la "Jehova Witness" hili dhehebu afadhali kidogo linafata mafundisho ya Yesu,lakini yaliyobakia yanahemkwa tu,samahani Mkuu sijui wewe uko dhehebu gani
 
Neno 'Sunnah' ina maana gani? Na neno Mutahab ina maanisha nini?
Neno "Sunnah" maana yake ni kufuata yale yote aliyofanywa na mtume Mohamad na Masahaba(watu waliokuwa karibu na Mtume) wake..
 
Achana nae ila nipe namba yake me ni Muslim tutaendana

Patience123
Chaaa...long time sijaingia Jf mumy.

Huyu namshauri asibadili dini kwa jina la ndoa,ipo siku atajutia uamuzi wake...

Vinginevyo sisi ni washauri tu,maamuzi anayo yeye. Asante kwa kunitag mamiake..
 
Waislamu Na wakatoliki Ni iman zao sawa tu haina shida
 
Chaaa...long time sijaingia Jf mumy.

Huyu namshauri asibadili dini kwa jina la ndoa,ipo siku atajutia uamuzi wake...

Vinginevyo sisi ni washauri tu,maamuzi anayo yeye. Asante kwa kunitag mamiake..
Abadili tu akizinguliwa si anarud tu alipotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…