Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

Ni sahihi mimi nitoke kwenye Ukatoliki niwe Muislam?

so mnashauri nibadili dini
Usibadili dini kwa ajili hiyo, unaweza kubarikiwa ndoa yako (Ndoa ya Imani tofauti). Msingi nenda kwa Paroko, atakwambia ujaze fomu na kisha atazituma kwa Askofu badaye utaruhusiwa kufunga ndoa ya DINI TOFAUTI yaani "Disparity of Cults".... Kila mtu atabaki na imani yake. Tatizo litakuja kwa watoto manake Moja ya mashariti ya ndoa hizi ni kuwa watoto wawe wakatoliki.

Ikishindikana tafuta Mkatoliki Mwenzako BUT kubadili dini hapana!!!!!
 
Usijaribu kubadilisha dini kumfuata mwanaume. Kesho akibadilika itabidi umfate atakapoenda.
Kuna ndoa ya bomani pia.
Kama ipo ipo tu.
 
Yesu ni njia na kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila.....angali kuna roho inakufuatilia,kama wazazi wamekukatalia wasilikilize wazazi.
Hao wazazi kama wamepotea nami ndio nipotee? Maswala ya dini wazazi hayawahusu ni wewe mwenyewe tu. Dini hairithiwi.
 
Nachojua mimi muislam akimbadilisha dini mwanamke kwa wanavyoamini wao anapata thwawabu zaidi that's why hawajipi muda kukuchunguza kama una tabia mbaya au la anacho-focus yeye ni tofauti na mkristo.

Mkristo yeye anataka akuchunguze tabia zako zote usije ukamletea mapicha picha ndoa zenyewe zile hazivunjiki tofauti na muislam ukizingua kidogo tu anakupiga talaka kwenu!!!..

Mwisho wa siku ni wewe na moyo wako na wazazi wako na kwanini unakimbilia sana kuolewa?au maisha mtaani yamekuwa magum sana maana hii nayo nasikia imekuwa ticket ya wanawake wengi kuolewa bila kujali wanaolewa ktk taratibu gani.
 
ndugu nakuombea kwa MUNGU aliye hai akupe neema ya kuijua kweli ili uwe huru, yaani mtu anakuambia MUNGU hana mtoto kwasababu hajawahi oa, hivi unadhani MUNGU WA KWELI kwa uweza wake anahitaji aoe ili apate mtoto? yaani aliyesema iwe dunia na ikawa unamfananisha na mwadamu kama wewe ambaye ili uwe na mtoto unahitaji mwanamke? kama hauamini kuwa YESU NI MWANA WA MUNGU ALIYE HAI NA KUWA ALITOLEWA MSALABANI MARA MOJA ILI ATUPATANISHE NA MUNGU, BASI UNAPOTEA
Mkuu poa,hiyo ni imani yako,wala mimi siipingi,mimi nasoma biblia,katika biblia hakuna hata kipande kimoja kinachosema kuwa Yesu(aka Isa aka Iso aka Yoshua) kasema kuwa yeye ni Mungu aabudiwe au yeye ni mtoto wa Mungu, au aombewe akiwa msalabani,au aitwe Yesu,

Najua kuna kipande kinasema kuwa Yesu alitahiriwa siku nane baada ya kuzaliwa,malaika walimpa jina la Yesu wakati akiwa tumboni mwa mama ake.,Yesu akapelekwa sehemu ya kuabudiwa ili aombewe...hivyo ndivyo biblia inavyosema...

luka 2:21
"Hata baada ya siku nane, ilipotimia siku ya kumtahiri mtoto, aliitwa Yesu; jina alilopewa na malaika kabla hata haja chukuliwa mimba.."

Red hayo imeyandika na kusema wewe mimi nahishimu dini ya kila mtu hata wale wanaoabudu miti,kama umesoma hizo comments zangu hakuna hata sehemu moja nimeisema dini ya Kikristo vibaya,..

Pale yule aliesema kuwa dini ya kiislam inaambudu mashetani na majini,hata hivyo ile comments niliijibu kwa muuono wa imani yangu ya kiislam..
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka kama mazuri jaman
 
USIBADILI DINI KISA UMEPATA MUME MUISLAM. BADILI DINI IKIWA UNAPENDA KUWA MUISLAM.UKIBADILI DINI ILI UOLEWE NI SAWASAWA NA KUOLEWA KWA KUFUATA MALI. UISLAM NI ZAIDI YA UNAVYOFIKIRIA AU KUONA WATU WAKIPRACTISE. UISLAM DINI NGUMU KAMA HUNA IMANI ILA VERY SIMPLE KAMA UNA IMANI. WELCOME TO ISLAM.
 
hiv mbinguni wanandoa mnabeba msalaba mmoja wa dhambi au kila mtu kivyake.........!!!??? hivi dini ni kigezo mbinguni?? afu huu utaratibi wa kufunga harusi kwa wapenzi ni official mpka kwenye vitabi vya dini?? au tumeanzisha wanadamu???.

Nipate majibi hayo tafadhar ili nimshauri vzur dada angu
 
Nachojua mimi muislam akimbadilisha dini mwanamke kwa wanavyoamini wao anapata thwawabu zaidi that's why hawajipi muda kukuchunguza kama una tabia mbaya au la anacho-focus yeye ni tofauti na mkristo.

Mkristo yeye anataka akuchunguze tabia zako zote usije ukamletea mapicha picha ndoa zenyewe zile hazivunjiki tofauti na muislam ukizingua kidogo tu anakupiga talaka kwenu!!!..

Mwisho wa siku ni wewe na moyo wako na wazazi wako na kwanini unakimbilia sana kuolewa?au maisha mtaani yamekuwa magum sana maana hii nayo nasikia imekuwa ticket ya wanawake wengi kuolewa bila kujali wanaolewa ktk taratibu gani.
Mkuu,sheria za kiislam zinaruhusu mwislam kumuoa mwanamke wa dini aliyekuja nayo Moses(Musa),Yesu(Isa), bila ya mwanamke kubadilisha dini..

Watu wanaofuata dini ya Yesu na Moses kiislam wanaitwa "ahalil kitabu",tafsiri yake ni watu wa vitabu,maana yake waisalam wanaweza kuoa wanawake zao kula vyakula vyao,kwani uisalm ni mwendelezo wa dini wa walizokuja nazo..

Lakini mwislam hawezi kumuoa mwanamke anaefata "biblia",mwislam anaweza kumuoa mwanamke anaefata "Injili",kitabu alichukja nacho ISA(Yesu),tafakari ujue kuna tafauti ya "Biblia" na "Injili"..
 
naombeni ushauri mimi ni msichana ambaye kwa muda sijawa na mtu nilitangaza hapa nimepata mtu nimempenda amenipenda.
ila sasa kazi ipo yeye ni muislamu.
naanataka nibadilishe dini.
kwetu ni nope .
ni imani tosha walishakata niolewe na dini tofauti kwao juzi tumeenda hali ndio hiyo.
nimechoka kabisa.
naombeni ushauri.
maana wakristo hawatamkii ndoa ila nikipata waislamu.
wanadai ndoa fasta.
hata miezi sita hafikii.
so niko njia pandaa hadi now.
Zamani kidogo,pale Manzese Madizini kuna bi Mdada mmoja toka uchagani alielelewa katika Ukatoliki,alipataga Bwana kama wewe na Akasilimu...baada ya ndoa akuweza pata mtoto,hivyo akalimwa Talaka tatu!...
 
Mkuu poa,hiyo ni imani yako,wala mimi siipingi,mimi nasoma biblia,katika biblia hakuna hata kipande kimoja kinachosema kuwa Yesu(aka Isa aka Iso aka Yoshua) kasema kuwa yeye ni Mungu aabudiwe au yeye ni mtoto wa Mungu, au aombewe akiwa msalabani,au aitwe Yesu,

Najua kuna kipande kinasema kuwa Yesu alitahiriwa siku nane baada ya kuzaliwa,malaika walimpa jina la Yesu wakati akiwa tumboni mwa mama ake.,Yesu akapelekwa sehemu ya kuabudiwa ili aombewe...hivyo ndivyo biblia inavyosema...

luka 2:21
"Hata baada ya siku nane, ilipotimia siku ya kumtahiri mtoto, aliitwa Yesu; jina alilopewa na malaika kabla hata haja chukuliwa mimba.."

Red hayo imeyandika na kusema wewe mimi nahishimu dini ya kila mtu hata wale wanaoabudu miti,kama umesoma hizo comments zangu hakuna hata sehemu moja nimeisema dini ya Kikristo vibaya,..

Pale yule aliesema kuwa dini ya kiislam inaambudu mashetani na majini,hata hivyo ile comments niliijibu kwa muuono wa imani yangu ya kiislam..
YOHANA 14:8
8.Filipo akamwambia, Bwana utuonyeshe Baba yatutosha, 9. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwa pamoja nanyi siku zote wewe usinijue Filipo? aliyeniona Mimi amemwona Baba,basi wewe wasemaje utuonyeshe baba? 10. Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? haya maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

haya ni maneno ya YESU mwenyewe na yapo katika BIBLIA. na kumbuka quran inasema kwa yale yatakayowatatiza muwaulize watu wa KITABU(yaani BIBLIA).
 
Waislamu hukimbilia ndoa fasta maana hujua kuna talaka tofauti na ukristo, mpk ujitafakari. Dada yangu alibadili dini 2008 kutoka RC na kuwa mwislamu, wazazi walimkataza Ila akatishia kujiua ikabd wamwache. Miaka kumi badae mwaka huu katelekezwa Mwanza mwanaume yupo Dar anakula bata. Usikimbilie ndoa kwa kubadili dini, Bali endelea kumwomba Mungu wa kwako atakuja.
Huyo mwanamme aliemfanyia dada ako hivyo sio muislam huyo,huyo anaitwa muislam jina
 
nimewaza na kila mtu hadi padri kakataa nibadili kasema Mungu hakukosea niwe mkristo na nilaana kubadili dini ya mababu zako so niko njia panda kiukweli nimechoka kabisa.
Kwahiyo ukristo ni dini ya babu zako?
Acha hizo wew waafrika hatukuwa na dini hizo zililetwa tu.
 
YOHANA 14:8
8.Filipo akamwambia, Bwana utuonyeshe Baba yatutosha, 9. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwa pamoja nanyi siku zote wewe usinijue Filipo? aliyeniona Mimi amemwona Baba,basi wewe wasemaje utuonyeshe baba? 10. Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? haya maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

haya ni maneno ya YESU mwenyewe na yapo katika BIBLIA. na kumbuka quran inasema kwa yale yatakayowatatiza muwaulize watu wa KITABU(yaani BIBLIA).
Kweli,hata wewe undani ya baba(Mungu) kama utamfata na kumuabudu baba(Mungu)unavyotaka...

Alivyokusudua Yesu kumwambia Filipo kwa kiswahili cha kawaida:-

"Nyinyi mnataka nikuonyesheni Mungu,kama mtanifata mimi ndio mmemfata Mungu,kila ninachokisema sikisemi kwa nafsi yangu bali kimetoka kwa Mungu na nafanya kazi kwa ajili yake"..

Hamna sehemu Yesu aliyosema yeye ni mungu hapo,..Mitume yote ni watoto wa Mungu na wanafanya kazi za Mungu
 
naombeni ushauri mimi ni msichana ambaye kwa muda sijawa na mtu nilitangaza hapa nimepata mtu nimempenda amenipenda.
ila sasa kazi ipo yeye ni muislamu.
naanataka nibadilishe dini.
kwetu ni nope .
ni imani tosha walishakata niolewe na dini tofauti kwao juzi tumeenda hali ndio hiyo.
nimechoka kabisa.
naombeni ushauri.
maana wakristo hawatamkii ndoa ila nikipata waislamu.
wanadai ndoa fasta.
hata miezi sita hafikii.
so niko njia pandaa hadi now.
utajuta maisha yako yote. huu ni ushauri wa bure.
 
Kweli,hata wewe undani ya baba(Mungu) kama utamfata na kumuabudu baba(Mungu)unavyotaka...

Alivyokusudua Yesu kumwambia Filipo ni kwa kiswahili cha kawaida:-

"Nyinyi mnataka nikuonyesheni Mungu,kama mtanifata mimi ndio mmemfata Mungu,kila ninachokisema sikisemi kwa nafsi yangu bali kimetoka kwa Mungu na nafanya kazi kwa ajili yake"..

Hamna sehemu Yesu aliyosema yeye ni mungu hapo,..Mitume yote ni watoto wa Mungu na wanafanya kazi za Mungu
unakaribia kuijua kweli tatizo roho ya upotoshaji bado inakushikilia, ipo siku utaijua kweli kamili. jioni njema mpendwa
 
Back
Top Bottom