Mambo yote yameanza kutoka kwa Nabii Musa(Moses) pale alipoteremshiwa amri kumi,akashushiwa kitabu cha Taurat ..
Yesu(Isa),Mohamad hawa wote wamekuja kuyaendeleza mafunzo ya Taurat,..hawakuja na kipya,kuna mambo yameyazisha na kuna mambo wameyapunguza kutokana na Amri ya mwenye Mungu..
Yesu(Isa) Kheri na baraka juu yake,aliwambia wanafunzi na wafuasi wake wasimfikirie kwamba kaja kubalidilisha au Sheria(taurat),bali amekuja kuzidumisha..
Matayo 5:17
"Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria(Taurat) aa Musa na mafundisho ya manabii.bali nimekuja kuzisisitiza"
"Do not think that I have come to abolish the Law or the Prophets; I have not come to abolish them but to fulfill them."
----------------------------*-*-*-*-*-*-*-*-*-*-------------------------------
Hamna hata sehemu mujo katika comments zangu nimeandika kuhusu Tohara ya mwili,nimeandika kuhusu kukatwa govi(kutahiriwa),..,
Yesu alitahiriwa siku nane baada ya kuzaliwa,waislam wanatahiriwa vile vile,siku arobaini baada ya kuzaliwa,..Taurat(agano la zamani) sheria inasema watu wasile Nguruwe,waislam hatuli Nguruwe,wakristo nguruwe wanamshangalia...Yesu hakuwahi kula Nguruwe,wayahudi hawali nguruwe,..Taurati inasema nguruwe asiliwe.. soma
Walawi 11:1-7
"Pia nguruwe,kwa sababu ana ukwato uliopasuka naye ana mwanya kwenye ukwato, lakini yeye mwenyewe hacheui. Huyo si safi kwenu"
Nimesoma biblia yote sijaona sehemu ambayo Yesu kasisitiza wanafunzi wake au wafuasi wake lazima wabatizwe,isipokuwa nimesoma kwenye Matayo 3:13-17 kuwa Yesu alibatizwa na John mbatizaji kama tohora ya kujisafisha roho
Matayo 3:13-17
3 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yordani ili abatizwe na Yohana. 14 Yohana alitaka kumzuia akimwambia, “Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, mbona unakuja kwangu? ” 15 Lakini Yesu akamjibu, “Kubali iwe hivi kwa sasa; kwa maana inatupasa kutimiza haki yote.” Kwa hiyo Yohana akakubali.
16 Na Yesu alipokwisha kubatizwa alitoka kwenye maji, ghafla mbingu zilifunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua aka kaa juu yake. 17 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye
Kubatizwa sio mambo aliyoyahubiri Yesu,sio mambo ya msingi au ya lazima kama unavyofiki....
1. Agizo la Ubatizo ni La Msingi. Kwakua ubatizo ulitoka Mbinguni.
Mathayo 21:25
Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini?
Marko 1:5
Wakamwendea NCHI YOTE YA UYAHUDI, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao.
Luka 3:12
WATOZA USHURU nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi?
Mathayo 3:7
Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo MAFARISAYO NA MASADUKAYO wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
Marko 10:39
Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na UBATIZO NIBAIZWAO MIMI MTABATIZWA.
Mathayo 28:19
Basi, enendeni, mkawafanye MATAIFA YOTE kuwa wanafunzi, MKIWABATIZA kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Yohana 3:22
Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, AKABATIZA.
2.Torati alivyoifundisha Yesu ina mambo ambayo mmeyatangua. Soma kwa makini ukurasa mzima wa Mathayo 5. Yesu Mwalimu wa Waalimu Akiifundisha Torati.
Mathayo 5:
17/Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
44Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
3. Kuhusu ulaji wa nyama ya Nguruwe, hii ni topic ya Peke yake. Manake ina mengi ya kueleza. Nisikuchoshe usome wewe mwenyewe (Mathayo 5).
Q. PIA NIMEWAHI KUSIKIA kua KUKIWA HAKUNA NYAMA NYINGINE , mNARUHUSIWA KULA KITIMOTO KAMA KAMA KAWAIDA.? Je hii ni kweli? Na kama ni kweli ni kiasi gani?