Ni sahihi mkeo kukutumia text kama hii?

Kazi yake ni nini sasa?
Wakati mwingine sisi wanaume huwa tunaanzisha ugomvi kwa mambo madogo sana. Jambo kama hilo halihitaji hata akili ya la saba kuling'amua ila mnataka kuanza ku complicate.

Tena huyo mwanamke ni mstaarabu sana amekua honest si vizuri mtu amelala uanze kumsumbua kumuamsha otherwise labda kama kuna emergency ambayo itamuhitaji kufanya hivyo. Tuepushe maugomvi kwa vitu vidogo vidogo kama hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee kwani vitasa vina funguo moja ....? [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Boss Mimi ni mwanaume na siwaendekezi wanawake ila kwa hili namtetea huyo dada .


Kwa sababu hata Mimi binafsi nikilala huwa sipendi kusumbuliwa ....yaani mtu huko ulewe kwa starehe zako alafu uje utusumbue kutuamsha usiku tuharibu usingizi kisa starehe zako hiyo hapana.


Vitasa vinafunguo nyingi Sana beba yako nabaki na yangu
 
Mi naona yupo sahihi.. kumuamsha mtu aliyelala akufungulie sio fair
Yupo sahihi tena sana tu.Yani mama wa watu anakuwa na tension muda wote asilale ili kumfungulia mtu asiyejulikana atarudi saa ngp!Si sawa kabisa, hata mimi nisingemfanyia hivo.Ningebeba ufunguo saa ya kurudi nirudi nilale kimyaaa bila usumbufu. Huo u Mungu mtu si mzuri.
 
Hahahahahah hii ndoa ni ya Mwendokasi, sikiliza hii, umelala asubuhi halafu Wife ameamka anaandaa watoto, ukisikia anasema hivi "Yaani mnafikiri Mimi sichoki? Niamke niwaandalie Kila kitu halafu nyie mmelala tu, hata Mimi nachoka"! Ukisikia maneno kama haya anayesemwa ni wewe na sio watoto. Huhitaji kupaniki.....
 
Mwambie ampe Funguo Housegirl, uone huo ugomvi wake, Yuko radhi akeshe anakusubiri Hadi pakuche
 
Kazi yake ni nini sasa?
Kama mwanaume mwenzako nadiriki kukwambia kuwa una akiri finyu kuhusu mahusiano na ndoa kiujumla mkuu. Being submissive to you doesn't mean you should treat her like a house maid kwamba kilakitu anapaswa afanye yeye hata kama mpo wawili tu ndani ya nyumba. Yaani utoke huko kwenye starehe zako tena usiku na mlango ufunguliwe kila siku. Hayuko pale kukustarehesha kimapenzi tu bali furaha yako iwe yake, ya kwake iwe yako na karaha zote ziwe zenu wote.
 
Wewe na huyo jamaa yako maboya sana ndo maana mnashinda pamoja. Ndege wafananao ....

Nyie ndo mnaosema mke lazima afue nguo hata kama Kuna washing machines mkiamini mke ni mtumwa wenu.
Sasa mimi uboya wangu ni nini haswa mkuu?
 
Kufunguliwa mlango hata saa6 mchana ni ufala. Huna funguo? Hana shughuli zingine za kufanya? What's so special about kufunguliwa mlango na kwanini wewe unataka ugonge kwako?

Matatizo ya mitanganyika hayatatuliwi hata na katiba mpya.
Kwa hiyo niwe natembea na funguo tu mfukoni kisa mwanamke hawezi fungua mlango??? hujafunga mlango unapoondoka asubuhi funguo unatembea nayo ili iweje?? Haya ndo mambo mwanamke anakufokea tu kifalaaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…