✓ Wakati mwingine funguo inaweza kupotea kisha ikawa msala kwa aliyefungiwa mlango kwa nnje kwa ATHARI zifuatazo;
1. Mke anaweza kuhitaji msaada wa ghafla ikiwa anaumwa na msaada zaidi wa karibu ukawa ni mumewe lakini bahati mbaya mtendao wa simu usiwe vizuri.
2. Anaweza kuzidiwa akashindwa kujikongoja hadi kufungua geti ili apate msaada hata toka kwa Jirani au kwa wapita njia.
✓ "Usumbufu" inamaana kurudi kwa Mumewe ni kero kwake ilihali usikute ni yeye mwenyewe ndiye sababu ya Mumewe kurudi usiku sana home tokana na gubu.
✓ Haiba ya kike huanzaga kuondoka kwa jinsi ujumbe unavyowasilishwa kwa Mumewe kwa lugha isiyo rafiki kimahusiano maana Me yeyote ajitambuaye hupenda utii toka kwa Mke.
✓ Watu wengi wameandika kimuhemuko bila ya kuangalia upande wa Me unasababishwa na ulazima upi hadi awe anamgongea Ke wake kufungua geti.
✓ Me anaweza kuajiri House Girl akawa anatelekeza yote kisha akawa Mke mwenza wa huyo Mke halali wa ndoa sababu ya uvivu wa kijinga.