Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Muziki wa Walokole na Wasabato kwenye bus ndio unachangamsha sasa, kwaya za Wakatoliki au Qaswida za Kobaz za Kiarabu hazifai kwenye bus sababu hazina vibe.
Hahaha za walokole hazina utulivu wa akili bwashee 😁
 
Muziki wa Walokole na Wasabato kwenye bus ndio unachangamsha sasa, kwaya za Wakatoliki au Qaswida za Kobaz za Kiarabu hazifai kwenye bus sababu hazina vibe.
Jadili mada, ukiwekea hizo za katoliki na kobaz ni sawa?🤣🤣
 
Kuna tabia imekithiri ya Bus zinazoenda mikoani hasa zinazomilikiwa na ndugu zetu wakristo kulazimishia abiria maudhui kwa kuweka nyimbo za injili, hasa mwanzo wa safari. Je hii ni sawa? Hasa ukizingatia sio abiria wote ni wa imani ya kikristo na hii huwa adha kubwa kwa wasio wakristo.

Nadhani waige mfano wa kampuni mbili kubwa za Bus, moja ya Morogoro na nyingine ya Gairo. Ukipanda zile Bus huwezi jua mmiliki ni wa dini gani au dereva na kondakta ni wa dini gani. Na hiyo ndio Tanzania

Ila ukipanda hizi za wachaga na wakinga kama sio mkristo utaita maji mma🤣🤣
Na hasa ukipanda basi za kwenda Mbeya, Njombe
 
Na hasa ukipanda basi za kwenda Mbeya, Njombe
Mama weeeešŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ¤£šŸ˜Ž, huko umepanda kanisa sio bus

Jaribu za Arusha na Moshi sasa nilizowahi kupanda(BM,Tilisho, Esther,Kilimanjaro) kwa
 
Utaratibu wa huduma kwa umma uko wazi unajulikana, aina yoyote ya ubaguzi kwenye huduma za umma hairuhusiwi ikiwepo na ubaguzi wa kidini🤣🤣
Basi wachukuliwe hatua za kisheria wenye hayo mabasi. Na sisi abiria tusikae kimya tupaze sauti.

Inakera sana huwezi kumwekea mtu wa imani tofauti qaswida au injili

Hata mimi sipendi kuona mtu wa imani tofauti na yangu anawekewa mahudhui ya imani yangu
 
Basi waambie watangaze kuwa kwenye bus lao kuna maudhui ya kikristo tu au ya kiislamu tu ili tusipande kabisa. Na sio kusubiri tumepanda ndo wafanye wanavyotaka, na ndio maana mwanzo kabisa tumesema kulazimisha maudhui.

Na pia wewe na uwezo wako mdogo wa kuchambua mambo ufahamu kuwa ule ni usafiri wa umma sio kanisa au msikiti🤣🤣 Kwahiyo unapochangia mada zinazohitaji akili kubwa changia ukiwa na akili zote
Ni kama zanzibar tu kipindi cha ramadhan hautakiwi ule hadharani hata kama sio muislamu....kuna mtu aliwahi kuleta mada kuhusu azam kuweka movie zenye maudhui ya kiislamu ambazo ni za vita kati ya waislamu na wakristo ila wachangiaji humu walidai kuwa haulazimishwi kuangalia azam tv
 
Back
Top Bottom