Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Ni upumbavu sana kwenye usafiri wa umma kuweka mahudhui ya kidini.

Maana mule kuna mchanganyiko wa imani mbalimbali. Wengine wanakwazika
Hii dunia ukiishi kwa kukwazika utaona maisha ni magumu. Kuna mwingine akiona bongo movies au akisikiliza bongo fleva ndani ya basi naye anakwazika.
Haya maisha huhitaji kuwa mtu wa complications
 
Angalau hayachagui imani ya mtu,

Mimi mwenye huwa sio mfuatiliaji wa hizo mambo nikiwa safarini. Huwa niko busy na simu yangu

Na kutazama nje huwa napenda sana kuangalia mandhari na mifumo ya maisha ya watu
Kwa waislam na walokole bongofleva ni haram! Haina mrengo wa Imani flani lakini ni kero kumsikilizisha mtu ambaye kwake ni haram
 
Nyimbo za injili zina shida gani?Zinatukana? Zinahamasisha vurugu? Zinahamasisha mauji? Zinahamasisha wizi? Mbona sijawahi sikia mkilalamikia nyimbo za bongofleva zenye maudhui ya ngono zinapopigwa kwenye mabasi?
Wewe kinachokupa furaha kuna mwingine kinamkera and vice versa is true. Haya maisha tunapaswa kuishi kwa kuvumiliana full stop
Mchango wako umepokelewa na wanajamii forum, ila kumbuka ule ni usafiri wa umma sio kanisa au msikiti🤣🤣.

Kama mawazo yako ni sahihi himiza nchi maeneo ya umma kisisikilizwe wala kuangaliwa kitu kingine isipokuwa injili🤣🤣. Tuone huo uvimilivu kama utapewa na watanzania
 
Kwa waislam na walokole bongofleva ni haram! Haina mrengo wa Imani flani lakini ni kero kumsikilizisha mtu ambaye kwake ni haram
Mambo ya imani ni complex ndo maana tunashauri watu waheshimu imani za wengine kwa kutokuweka imani zao juu ya zingine kwenye maeneo ya umma(kama kwenye bus)😎😎
 
Nyimbo za injili zina shida gani?Zinatukana? Zinahamasisha vurugu? Zinahamasisha mauji? Zinahamasisha wizi? Mbona sijawahi sikia mkilalamikia nyimbo za bongofleva zenye maudhui ya ngono zinapopigwa kwenye mabasi?
Wewe kinachokupa furaha kuna mwingine kinamkera and vice versa is true. Haya maisha tunapaswa kuishi kwa kuvumiliana full stop
"Full stop" unaiweka tu🤣🤣, sio kuiandika. Hauna mamlaka ya ku-override mawazo na maamuzi ya watu wengine toa mchango wako tu watu waamue kuusikiliza au la, kama kuna maoni kinzani utapewa hoja na wewe ujibu
 
Nyimbo za injili zina shida gani?Zinatukana? Zinahamasisha vurugu? Zinahamasisha mauji? Zinahamasisha wizi? Mbona sijawahi sikia mkilalamikia nyimbo za bongofleva zenye maudhui ya ngono zinapopigwa kwenye mabasi?
Wewe kinachokupa furaha kuna mwingine kinamkera and vice versa is true. Haya maisha tunapaswa kuishi kwa kuvumiliana full stop
Hatutamani kujadili uhalali au ubaya wake🤣, sio lengo la hii post hiyo shughuli wataifanya mashehe na wachungaji🤣
 
Hii dunia ukiishi kwa kukwazika utaona maisha ni magumu. Kuna mwingine akiona bongo movies au akisikiliza bongo fleva ndani ya basi naye anakwazika.
Haya maisha huhitaji kuwa mtu wa complications
Huwezi kutupigia nyimbo za injili au kaswida njia nzima safari ya masaa kumi na mbili afu tukikwambia utuite watu wa complications🤣🤣, jadili hoja kwa hoja na sio kutulazimishia uvumilivu kwa kitu kilichopo ndani ya uwezo wako kutuhudumia wateja wako.

Miongozo iko wazi, ubaguzi wa aina yoyote kwenye kutoka huduma za jamii hauruhusiwi, kwahiyo pia kutuambia tukapande ambayo haipigi hizo ni kosa. Kama huamini ni kosa waambie waandike mlangoni kuwa wanapiga gospel tu kama haupendi usipande au asietaka asipande uone kama watapewa leseni ya usafirishaji😎😎
 
Sasa c unaona bado tunarudi kule kule kuwa Huwez kumridhisha kila mtu, Au hayo magari yamewekwa kwa ajili ya Wakristo na Waislamu tuu?
Nyingi zina TV, hivi kweli duniani hamna cha zaidi cha kuonyesha ksichohusiana na imani ya dini yoyote🤣🤣, mbona unawatetea kisirisiri.
Tuambie unasapoti wanavyofanya au wabadilike?😀
 
Kuna tabia imekithiri ya Bus zinazoenda mikoani hasa zinazomilikiwa na ndugu zetu wakristo kulazimishia abiria maudhui kwa kuweka nyimbo za injili, hasa mwanzo wa safari. Je hii ni sawa? Hasa ukizingatia sio abiria wote ni wa imani ya kikristo na hii huwa adha kubwa kwa wasio wakristo.

Nadhani waige mfano wa kampuni mbili kubwa za Bus, moja ya Morogoro na nyingine ya Gairo. Ukipanda zile Bus huwezi jua mmiliki ni wa dini gani au dereva na kondakta ni wa dini gani. Na hiyo ndio Tanzania

Ila ukipanda hizi za wachaga na wakinga kama sio mkristo utaita maji mma🤣🤣
Ni sawa kabisa mkuu. Ni afadhali kuweka nyimbo za injili au kaswida kuliko hizi nyimbo za akina Dayamondi zinazotukuza bangi na ngono. Au wewe unapenda ngono na bangi mkuu?
 
Hii dunia ukiishi kwa kukwazika utaona maisha ni magumu. Kuna mwingine akiona bongo movies au akisikiliza bongo fleva ndani ya basi naye anakwazika.
Haya maisha huhitaji kuwa mtu wa complications
ndo utuwekee injili au kaswida??🤣🤣
Ni sawa kabisa mkuu. Ni afadhali kuweka nyimbo za injili au kaswida kuliko hizi nyimbo za akina Dayamondi zinazotukuza bangi na ngono. Au wewe unapenda ngono na bangi mkuu?
Sio sawa🤣

"kwa waislamu yesu sio mungu, Kwa wakristo Yesu ni Mungu"

Na kwenye hiyo bus kuna abiria wa dini zote🤣
 
Ni sawa kabisa mkuu. Ni afadhali kuweka nyimbo za injili au kaswida kuliko hizi nyimbo za akina Dayamondi zinazotukuza bangi na ngono. Au wewe unapenda ngono na bangi mkuu?
Ndio, ila siwezi kulazimisha usikilize maudhui yake hadharani kwenye maeneo ya umma hata kama hauhitaji
 
Ndio, ila siwezi kulazimisha usikilize maudhui yake hadharani kwenye maeneo ya umma hata kama hauhitaji
Exactly. Hata mm naona afadhali kusikiliza kaswida/injili au hata mawidha ya kiislamu/kiinjili kuliko hizi nyimbo za ngono na bangi. Hakuna kinachoniudhi naingia kwenye basi/daladala halafu nasikia nyimbo zinazotukuza bangi, ngono na uvunjivu wa sheria na zinapigwa kwa sauti kubwa. Inaniuma sana.
 
Back
Top Bottom