Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Muziki wa Walokole na Wasabato kwenye bus ndio unachangamsha sasa, kwaya za Wakatoliki au Qaswida za Kobaz za Kiarabu hazifai kwenye bus sababu hazina vibe.
Hahaha za walokole hazina utulivu wa akili bwashee 😁
 
Muziki wa Walokole na Wasabato kwenye bus ndio unachangamsha sasa, kwaya za Wakatoliki au Qaswida za Kobaz za Kiarabu hazifai kwenye bus sababu hazina vibe.
Jadili mada, ukiwekea hizo za katoliki na kobaz ni sawa?🤣🤣
 
Na hasa ukipanda basi za kwenda Mbeya, Njombe
 
Utaratibu wa huduma kwa umma uko wazi unajulikana, aina yoyote ya ubaguzi kwenye huduma za umma hairuhusiwi ikiwepo na ubaguzi wa kidini🤣🤣
Basi wachukuliwe hatua za kisheria wenye hayo mabasi. Na sisi abiria tusikae kimya tupaze sauti.

Inakera sana huwezi kumwekea mtu wa imani tofauti qaswida au injili

Hata mimi sipendi kuona mtu wa imani tofauti na yangu anawekewa mahudhui ya imani yangu
 
Ni kama zanzibar tu kipindi cha ramadhan hautakiwi ule hadharani hata kama sio muislamu....kuna mtu aliwahi kuleta mada kuhusu azam kuweka movie zenye maudhui ya kiislamu ambazo ni za vita kati ya waislamu na wakristo ila wachangiaji humu walidai kuwa haulazimishwi kuangalia azam tv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…