Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Shetani peke yake hapendi kusikiliza ama kutazama habari njema za Mungu,mashetwaini ma majini ,mawakala wa kuzimu ndio hawapendi kusikia habari za Mungu..njema za Mungu.
 
Uislamu na ukristo ni ujinga wenu mliouanzisha wanadamu.

Kitakachokupeleka mbinguni ni matendo mema sio ukristu au uislamu wako.
usiite watu wajinga, ukitukaniwa mungu wako utajaza povu🤣🤣..changia mada kama ilivyowasilishwa tutapokea mchango wako na kukubali mawazo mbadala
 
Issue sio dini,
Wote tuna abudu Mungu, Sasa ikipigwa nyimbo ya kikristo au ikipigwa hadithi za Quran sio issue ilinradi zinatoa mafunzo
Tubapishana padogo tu
 

Unataka waweke nyimbo zipi? Wakikukera acha kupanda buses zao
 
Waislamu hawataki dominace ya ukristo iwe kwa namna yeyote.....
Utakuta mmiliki wa Basi ni mwislamu ila ndani ya basi lake amejaza nyimbo za gospel.............
Yupo sahihi tu kwasab hao ni wateja wake..........
Mbona wasanii na wanamichezo wengi kwenye nchii hii ni waislamu kwa 60% na Wakristo hawana tatizo na hilo, na ni fans wao.
 
Unataka waweke nyimbo zipi? Wakikukera acha kupanda buses zao
Tunatamani hivo, andikeni kwenye matangazo kwamba ndani ya hizo bus ni injili injili au kaswida mwanzo hadi mwisho wa safari ili tusipande kabisa tusiwakere na bus zenu🤣🤣
 
Issue sio dini,
Wote tuna abudu Mungu, Sasa ikipigwa nyimbo ya kikristo au ikipigwa hadithi za Quran sio issue ilinradi zinatoa mafunzo
Tubapishana padogo tu
Sio wote tunaabudi mungu, unakosea🤣🤣
 
Unalazimishwa kufanya nini mkuu
 
Hatupo huko😊, umeenda nje ya mada ili kugawa watu kwenye comment kiimani🤣🤣, au labda hujaelewa mada ngoja nikurudishe utupe mchango mzuri.. ni sahihi ndani ya bus njia nzima inapiga nyimbo za injili tu wakati abiria waliopanda ndani ni wa dini mbalimbali?
 
kwahiyo wewe unataka dominance ya imani yako kwenye bus sio? 🤣🤣 basi sawa, tunajifunza mengi yaliyojificha kwenye hizi comments pia🤣🤣🤣🤣😊😎😎
 
una point imehificha unaogopa kuisema tu, hebu jikaze uitoe tupate maoni yako🤣🤣🤣😎😊
 
Shetani peke yake hapendi kusikiliza ama kutazama habari njema za Mungu,mashetwaini ma majini ,mawakala wa kuzimu ndio hawapendi kusikia habari za Mungu..njema za Mungu.
Sawa malaika🤣, uko peponi kwa mungu wako unalazimisha watu wote wawe kama wewe🤣🤣
 
Shetani peke yake hapendi kusikiliza ama kutazama habari njema za Mungu,mashetwaini ma majini ,mawakala wa kuzimu ndio hawapendi kusikia habari za Mungu..njema za Mungu.
point ni wewe kukaa na umalaika wako, usitulazimishie kuusikiliza utakatifu wako🤣🤣, ukitaka tuupate umalaika wako utuombe ridhaa kukusikiliza sio ulazimishe tukusikilize. M

sisi katika utiifu,
Mashetani(kwa uelewa wako finyu)🤣🤣🤣🤣
 
nakufafanylia ili uelewe naona huelewi au unabadilisha mada makusudi.

sasa hebu jaribu kufikiri siku umeenda kuangalia simba au yanga, afu muda wote uwanjani zinapigwa kaswida tu, au injili tu🤣🤣🤣? Ni sawa hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…