Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Ukish
Ukianzisha biashara za umma,yaani wateja wako ni mtu yoyote yule,ni vyema ukawa neutral kwenye masuala ya imani za kidini ili uwape furaha wateja wako.Huo ndio msimamo wangu japo siwezi kumuingilia mtu na mali zake
 
Inategemeana na imani ya dini ya dereva na konda wanapendelea kuweka nini. Waislam huweka maudhui ya kiislam, wa kidunia huweka miziki na filamu za kidunia. Kuna mabasi ya kigogo mmoja mkubwa hapa nchini huwekwa picha za maumbile ya dunia/land scape nature tu, mwanzo mwisho utaona filamu ya mazingira tu. Mi husafiri na miziki na muvi zangu kwenye simu/ipod ili nikikutana na miziki/muvi za kwenye mabasi nisizozipenda basi naangalia zangu, nasikiliza miziki yangu kwa kutumia bluetooth/earphone, silazimiki kusikiliza miziki na kuangalia filamu za kwenye mabasi nisizozipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…