Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Ni sawa kuweka nyimbo za injili kwenye mabasi ya mikoani?

Muwe mnasafiri na miziki yenu, hamlazimishwi kusikiliza miziki mnaoikuta imewekwa. Mnakera sana, mara ooh punguza sauti, sie wengine tunapenda miziki hiyo, tena kwa sauti kubwa!
Panda kanisa sio public transport, au nunua gari yako sio utulazimishe tusikilize unachotaka wewe afu tumelipa nauli sawa na uliyolipa wewe🤣🤣
 
Hii mada haihusu tu gospel songs hata wale wapiga qaswida nao wanafeli kama wenzao wa nyimbo za injili
Ni kweli, ila sidani kama waislamu huwa wanahangaika kulazimishia watu qaswida au maudhui ya dini kwenye bus. Binafsi sijawahi kuona bus iliyoweka maudhui ya kiislam, kama ipo haitakiwi pia
 
Hayo nafikiri ni maamuzi binafsi ya mwenye usafiri kama unaona ni kero kwako unaweza kutafuta usafiri utakaokuwa na maudhui uyapendayo
Mkuu, ukishaamua kuingia kwenye biashara ya kuhudumia umma, mambo ya ''maamuzi binafsi'' yamawekwa pembeni na kinachotangulia ni ''matakwa ya umma''. Mimi naenda mbali zaidi na kusema mabasi hayatakiwi kupiga muziki wa aina yoyote kwa sababu siyo kila abiria anataka kupigiwa kelele. Kama unahamu ya kusikiliza chochote, beba simu yako na earphone.
 
Kuna mmbaba mmoja alikuwa amevalia kiislam, tuko kwenye basi akaamuru konda azime tv, alionesha kukerwa na miziki ya kidunia ya kina diamond, zuchu, marioo, ally kiba, rayvanny, jux, mbosso, aslay, harmonize na wengine wengi wa bongo fleva huku sie wengine tukifurahia miziki hiyo safarini. Abiria mmoja hawezi kuzuia wengine wasiendelee kuburudika safarini ndani ya basi. Ni bora alale tu kuliko kukera abiria wenzake wanaofurahia miziki hiyo ndani ya basi
 
Kuna tabia imekithiri ya Bus zinazoenda mikoani hasa zinazomilikiwa na ndugu zetu wakristo kulazimishia abiria maudhui kwa kuweka nyimbo za injili, hasa mwanzo wa safari. Je hii ni sawa? Hasa ukizingatia sio abiria wote ni wa imani ya kikristo na hii huwa adha kubwa kwa wasio wakristo.

Nadhani waige mfano wa kampuni mbili kubwa za Bus, moja ya Morogoro na nyingine ya Gairo. Ukipanda zile Bus huwezi jua mmiliki ni wa dini gani au dereva na kondakta ni wa dini gani. Na hiyo ndio Tanzania

Ila ukipanda hizi za wachaga na wakinga kama sio mkristo utaita maji mma🤣🤣
Wanakera sana hawa mbwa! Ingekuwa Bus za waislam wanaweka mawaiza ya kiislam au Qur'an,wangelalama Nchi nzima
 
Back
Top Bottom