Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 8,423
- 29,012
Nadhani huwa hawajui kuwa zile TV ni kwa ajili ya abiria na sio wao makonda na madereva..Watu wengi wa usafirishaji hawajui kuwa abiria wengi wanaosafiri wanahitaji utulivu katika safari zao, wapo wanaoenda misibani, wengine kwenye usahili, hivyo kwa kiasi kikubwa safari inatakiwa kuwa na utulivu. Lakini wao wanaweka mamuvi au manyimbo yaani makelele tu, hadi mtu unakosa utulivu wa kutafakari mambo yako ya msingi. Wasichokijua ni kuwa vitu vyote wanavyoweka kwenye tv za kwenye mabasi sisi huwa tunaviona majumbani kwetu kwahiyo hatuna interest navyo kabisa. Mimi nainjoi safari kwenye gari ambalo tv imezimwa kwakweli.
Lakini pia sometimes kwa safari ndefu. Kheri waweke tu hizo destructions japo sauti wakicontrol itakuwa sawa zaidi kwa watu wasio interested..