Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Tabora Kuna sehem Moja Kuna njia panda ya kwenda mpanda na barabara lingine linaingia maporini......Picha linaanza mwenyeji alokuja kutupokea usiku mwenyewe alitupoteza, pili hatukua tukiona nyumba Wala chchte ni Giza tu......Tumesogea mbele tukashuka kweny gari kuangalia tuelekee usawa gani katokea bonge bonge ya joka tukakimbilia kweny gari tukaanza tena kuitafuta njia tukaipata

Tulivofika hapo msibani tukala tukala usiku nmelala nasikia kitu kikubwa kipo mgongoni kwangu kuwasha tochi nakutana na panya analinga a kichwa na Putin. Weeeh nlipiga kelele watu wote wakaamka nduki
Asubui nmeamka wakasema tuende tukapaone sehem alipozikwa ndugu yetu tukafika tukaanza kurudi nyumbani tukakutana tena na joka nlikua natetemeka hadi nikaingia period

Tukarudi nyumbani muda wote natembea sion nyumba za watu nkajiuliza Ina maan huku watu wanatokea wapi kumbe huko ndani ya msitu zaid

Siku tunarudi tukakutana barabarani na fisi mara na mbwa mwitu mara nyoka kakaa katikati ya barabara eeeh nyumba tukaona chache sana zenyewe ziko mbali mbali
Tulivofika center bwana weeeh nilijikuta nipo hospital maan nlikata moto gafla baada ya kusema tumbo linauma

Nilijiuliza watu huko wanaish vp, nyoka kila Kona, fisi mbwa mwitu,wanakunywa maji meupe kama maziwa, hospital ni mbali kias kwamba lazima uombe Pooh
 
Kijiji cha Gamboshi kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Ntarudi.
Kutoka Bariadi mjini unapita kijiji cha Ngulyati kiasi cha kilometa 30 Mashariki ya Bariadi katika barabara itokayo Bariadi kwenda Magu, lakini hakuna kibao kinachotambulisha Kijiji cha Gamboshi mwanzoni mwa barabara ya vumbi inayoelekea Gamboshi kutoka Ngulyati.

Upande wa kaskazini kijiji hicho kinapakana na kijiji cha Kisesa kilichopo wilaya ya Busega, kusini kinapakana na Nyamswa, Magharibi kijiji cha Lulayu, kusini- Magharibi kijiji cha Ditima na Mashariki kijiji cha Miswaki.

Wananchi wa kijiji hicho ni wacheshi, wachapa kazi na wanajali wageni kwa kuwapa historia ya kijiji hicho huku wakitumia nafasi hiyo kuwaondolea dhana iliyojengeka kuwa ni kijiji cha wachawi.
 
Hizi period za mwendokasi zinatishia afya ya dada zetu
 
Kuna kijiji huko dodoma walishambulia watafiti.
 
Poleeee 🤣🤣🤣
 
Mpwapwa kwa ujumla tu sijawahi kabisa kupaelewa.
 
Ukitokea W .Mkalama ukipita daraja la sibiti kwenda kutokea Meatu Kuna Kijiji baada ya Daraja la sibiti ambalo limeshakamilika ujenzi asee wale watu is so special tulikuta ngoma pale asee vitoto umri around 16 /20 vinacheza chuchu hazarani ..hakika iyo siku mkuyenge ulipata tabu sana
 
Mkuu 😂😂😂
Mimi nina picha kabisa za hivyo vijiji nimefika huko yaani sehemu hata baskeli haifiki. Usafiri ni mitumbwi tu.
Niliwauliza hivi mnajua rais wa sasa hivi ni nani? Wakasema samia nikasema mmejuaje maana huku tv hamna wala network hashiki😂
Sema yale mazingira ya ziwani mazuri sana kama unataka kufanya retreat ya kujitenga na watu. Ukijani na ziwa + milima milima.
Yaani mtu anaamka asubuhi anaenda kupia mswaki ziwani maana ziwa lipo umbali kama wa mita mia.

Hiyo ya kulima milimani nilishagaa sana maana wakati wa kushukainabidi uwe makini kweli kweli unaweza kuteleza na kuanguka bondeni huko.

Baada ya kwenda hilo eneo niligundua kwanini Wasanii wakipanda kilimanjaro huishia njiai.
Mimi napenda nature, nimetembea mapori mengi humu TZ na kujionea mengi
 

Sasa bosi hapo ni Bariadi... Ukiingia ndani kuna wilaya kama itilima nk. saa 11 fisi wanapiga misele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…