Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Nenda Morogoro shuka msamvu, chukua bodaboda akupeleke hadi shule ya msingi kikundi, nauli 1500.
Ukifika pale angalia mlimani kule watu wamejenga mlimani yaani. Sasa unajiuliza hawa watu hata mabati walipelekaje kule!
Kule ndio wenye hela wanajenga,kwa kishua kule,
Barabara zimechongwa safi. Gari yoyote inafika nila shida.
 
Asante ww ndo umeelekeza vzuri kabisa kabisa
 
Yani Mkuuu mim nikiona joka naweza Kata moto Ile siku sitasahau....... siku tatu nkaona mwezi
 
Msitu wa inyonga
Uzi mzuri sana, huko maporini inaonekana ndipo penye hela. I wish watu wa serikalini wangeona huu uzi labda wangeingiwa huruma kutafuta hivi vijiji na kupeleka services especially kuwachimbia visima vizuri vya maji na zahanati
Wapo busy kununua V8 lakini kutenga million 500 kujenga barabara ya changarawe au kuchimba visima hawana muda na pesa hizo
Such a useless general assembly
 
Zanzibar INA ukubwa gani?
 

Acha wivu wa kike hapa hatuzungumzii chakula
 
Mbona unaandika ujinga then haichekeshi
 
Uzi mzuri sana, huko maporini inaonekana ndipo penye hela. I wish watu wa serikalini wangeona huu uzi labda wangeingiwa huruma kutafuta hivi vijiji na kupeleka services especially kuwachimbia visima vizuri vya maji na zahanati
Watu wa serkali nani? Watu wapo busy kuipigania familia zao we endelea kubana pua watu wa serkali
 
Mkuu hukuona sehemu tambarare ukitoa sehemu zenye milima?
 
Nimecheka kwa kelele ha haaa.
 
Siku moja niko na jamaa yangu tunatafuta mashamba ya kukodi ya alizeti tulikua na mwenyeji anatutembeza mashambani. Mchana tunataka kurudi mwenyeji akatuambia twende kwanza kwake tule ndio tuondoke. Tukaona si mbaya.
Tumefika tukaenda sebuleni Chakula kikaja nikasahau kabisa kama Chakula chao kikuu ni mlenda.
Bwana bwana ulikuja ugali mgumu na mlenda mimi nilikua sijawahi kula mlenda wala ugali wa mtama😅

Nilihangaika mwenye ananiambia mbona hauli au chakula kibaya? Mimi naguna guna tu😂, nilishwindwa kula aisee ilibidi nikaupiga picha hii hapa chini.
Yaani utadhani unakula hina. Watu wanawakiwa na jua huko ndio maana miguu yao imekomaa halafu myembamba kama mianzi imechomekwa kwenye mapaja 🏃🏃
 
Narudia tena hakuna mkoa masikini kama Dodoma.

Mkoa ule ni hatari huko wilayani.

Nilienda huko Kijiji Cha Chimendeli wilaya ya Bahi, Kwanza hiki Kijiji ndio kinaongoza kutoa omba omba wengi Sana tanzania.

Familia zinashindana kuja mijini kuomba omba. Mzazi anaweza kumtuma mtoto wake aende mjini awe omba au mzazi anaweza kuja mjini na familia nzima waje kuwa omba omba!

Kwa ambao mko Dar Es Salaam kuanzia Leo jitahidi ukikutana na omba omba watoto au wazee wadadisi Kwa maswali halafu waulize wanatoka Kijiji gani. Halafu piga nao story hutakaa uamini !


Kama ulivyo kwenu vijana wanasoma Kwa jihadi zote waje kuwa Madaktari Ila kuna sehemu hii tanzania watu Wana ndoto za kuwa omba omba. Au kama hamuamini Ulizieni hata walimu WA Shule walioko hicho Kijiji. Watoto hawaendi shule.

Sehemu ni kame.


Lile eneo unaweza kudhan upo Pakistan au Kule Yemen.


Eneo lingini ni vijiji vya wilaya ya kongwa.


Acha niishie hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…