Yah ni kweli ata Zanzibar kuna maendeleo kushinda Tanganyika, Nimeishi Zanzibar sikuwahi kuona Wamama wakipata shida ya maji na huduma za hospitali na usafiri, umeme upo kila sehemu, sehemu zote za Tanzania Zanzibar hawana shida za huduma za kijamii huduma zote zimewafikia wananchi, tembea Zanzibar kote huwezi kukuta mama kabeba ndoo ya maji kichwani , na uko vijiji huduma zote zipo, yani Zanzibar kuna vitu vingi vya elektroniki mpaki vijijini, Zanzibar mtu kukupa nyumba uishi au kukuazima gari lake uendeshe ni jambo la kawaida tena uko ni mashambani.