Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

asande sana mkuu.
 
thanks alot bro, asande sana kwa maelezo yako,

ubarikiwe.
 
Sehemu nyingine ipo wilaya ya Mbalali mkoa ni Mbeya kule Blonde la Mpunga la Usangu. Kule kuna vijiji vingi Sana. Kuna Kijiji nilikaa pale Miezi nilishangaa Sana.

1. Sikuwahi kusikia Kuna kituo cha police au police . Kule bangi inavutwa kama sigara.

2. Kwa wale wala kitimoto kule inauzwa kama Dagaa.

3. Kwasababu kitimoto ni nyingi Sana na hawaoimi Kwa kilo wanaweka Kwa mafungo kama nyanya. Kitimoto ya 4,000 ukimaliza wewe ni shujaa.

4. Sikuwahi kuona limao, kitunguu , Ndizi za kuiva wala nyanya.

5. Hiyo kitimoto inapikwa Ila bila hivyo vitu hapo juu.


6. Usiku kuisikia Sauti ya wanyama wakali kama Simba na tembo ni kawaida.


7. Kuna Baridi usiku kama uko Yemen au Kwenye Vilima Vya magaidi wa Taliban kule Afghanistan.

8. Sikuwahi kuona kiwanja cha mpira hata kupiga danadana.


9. Kule mchele na wali unaweza Kula Hadi ufe hakuna Kijiji nimetembea tanzania nikakuta kina mchele kama kile.
 
Mwaka gani hii ilikuwa?
 
Kuna kijiji kipo Iringa ndanindani[emoji16][emoji16]

Asubuh nikaletewa maji ya kuoga nikaoga fresh sasa ilivyofika jioni nikasema ngoja niende na huyo dada nikachote mwenyew [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hicho kisima unachota maji pamoja na chura, unafanya kuwatoa chura kwenye ndoo ili upate maji aiseeh

Ikifika mida ya saa 12 jioni wanakijiji wote wanaenda kilabuni inshort kijiji kizima wanamwagilia moyo[emoji23]
 
Nimesafiri karibia mkoa mziam wa sumbawanga na katavi nilienda kijij kimoja kipo nkasi gerezani kule tulienda nikakuta kijij sijui ndio center watu Ni wakora kinyamaa wakta nacheki cheki Kama nitampata mwalifu tulio muendee nikaona ngoja nichungulie ndani Kuna kibanda kipo kipo naziona silaya nzito nzito ndani mle nikasema moyon muda wowote nitatandikwa risasi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mi pia nilishindwa kula huu mlen damwenzenuu Kaahh!!!
 
Uko sahihi 100%nakukubalia nimepitia vijiji vingi vya Dodoma ,Kuna umaskini wa kutisha
 
[emoji28][emoji28][emoji28]

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kuna kijiji kinaitwa lipalilo kule hakufai mwaka 2013 labda sahivi Kuna mabadiliko Ila mazingira ya wakinga magumu sana
Na Kuna Kijiji Cha utengule pembezoni mwa safu za milima ya Kipenge Mkoa wa Njombe Ni Kama Kisiwa wakinga wa kule wakitaka mahitaji wanakuja wilaya jirani ya Kyela sehemu hiyo inaitwa Ngyekye kupitia hiyo milima wakati huo nasoma Shule moja Matema Beach Sec Basi usiku unaona tochi hapo ujue ndo wanashuka Mnadani kufuata mahitaji hasa siku ya alhamisi. Utastaajabu mlima una urefu wa Mita 2600 lakini wanashuka madebe ya ngano kichwani au maharage ndipo auze halafu arudi na madebe ya mchele. Sisi tulipanda ule mlima tukiwa hatuna mizigo lakini tulichoka mpaka tulitoa jasho la njano. Jamaaniiiiiiii usimuliwe tu unakutana wamama mpaka wanavipara nywele zimenyonyoka ktokana na kubeba mizigo wakati huo anapanda mlima akiwa na andasket tu maziwa yote njenje Kama makilikili na hawashtuki. Duuuu Tanzania Ni Pana. Sijui walifuata nini Kule.
 
Lindi
 
Siku hizi huko network ipo powa sana.kijiji kinaitwa Mbaha,vingine ni Lundu ,Lituhi,Nkiri,Mango,nk asubuhi hakuna chai unapata mchemsho wa samaki au dagaa fresh na ugali wa unga wa mihogo
 
Wanyantuzu hao na mila zao

Ukifumwa na binti kule ngwekwe inakuhusu ( faini ) na wanakususia mtoto wao sijui utafanyaje maana nyengine ni za kutegesha

Wengi hawajasoma na hawajui kiswahili mtoto akisoma mahari za ng'ombe zinapungua kuogapa matatizo na serikali ndio maana wanaambiwa wajifelishe
 
Siku hizi huko network ipo powa sana.kijiji kinaitwa Mbaha,vingine ni Lundu ,Lituhi,Nkiri,Mango,nk asubuhi hakuna chai unapata mchemsho wa samaki au dagaa fresh na ugali wa unga wa mihogo
Yes , mbaha na huko kwengine na wenyeji wakarimu sana maeneo yote hayo tuliyozunguka muda wote tuliikuwepo walionyesha ushirikiano nasi na hata chakula wakajitolea kwa Hiari yao ni samaki,kuku,mbuzi na unga wa muhogo

Tatizo lilikuwa kwenye network tu na ilikuwa inashika MTN na radio za Malawi ,kingine lugha kwa wakazi ya maeneo yale

Mpakani Tz - Malawi walizoea kupita kama nyumbani kwao,mambo ya taratibu na Sheria baadhi walikuwa hawajui + athari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…