Siku moja niko na jamaa yangu tunatafuta mashamba ya kukodi ya alizeti tulikua na mwenyeji anatutembeza mashambani. Mchana tunataka kurudi mwenyeji akatuambia twende kwanza kwake tule ndio tuondoke. Tukaona si mbaya.
Tumefika tukaenda sebuleni Chakula kikaja nikasahau kabisa kama Chakula chao kikuu ni mlenda.
Bwana bwana ulikuja ugali mgumu na mlenda mimi nilikua sijawahi kula mlenda wala ugali wa mtama[emoji28]
Nilihangaika mwenye ananiambia mbona hauli au chakula kibaya? Mimi naguna guna tu[emoji23], nilishwindwa kula aisee ilibidi nikaupiga picha hii hapa chini.
Yaani utadhani unakula hina. Watu wanawakiwa na jua huko ndio maana miguu yao imekomaa halafu myembamba kama mianzi imechomekwa kwenye mapaja [emoji125][emoji125]
View attachment 2379797