Mongwe uukoNilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
acha kutosimanga mkuu...Kijiji cha Chimendeli, wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.
Sijui kule watu Wanaishi vipi. Unaweza Kudhani uko Somalia au Afghanistan.
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kwa kina muraa ni kawaida sanaaMkoa wa Mara wilaya ya Butiama
Hahah..hi ngoma ni kishiri kama sikosei
Tatizo statistics na calculation za kiuchumi haziangalii hivyo mkuu, ila kupitia uzi huu mimi mwenyewe nmekubali Tanzania ni kubwa balaaTanzania hii ni kubwa sana nashangaa watu kujilinganisha na Rwanda, na Kenya kimaendeleo wakati hizo nchi zinaingia mara mbili kwa Tanzania
Kupata kiberiti Lazima upande tandamu zinazobeba magogo uwape 1500 na kurudi 1500 jumla buku tatu kiberiti Cha mia
Dah, hiki kijiji cha kwenda kutembelea.Kijiji kingine ni mpyagula, kwa mbele kuna wasukuma wengi miaka ile wali na kambale mkubwa sana ilikua ni mia tano tu, mwenyeji wangu aliponiona kama nina mawazo akajadili na mke wake wakamwita binti mdogo wa mke wake aje anifariji chumbani na binti alikua mwanafunzi nilishangaa sana sitosahau hiko kisa
Ile milima na yale makazi na mvua zile za kanda ya ziwa, itoshe kusema Mungu ni mwema sanaSawa. Ila mwanza sehemu kubwa ni milima na mapango. Ni Mungu tu anawalinda wanaMwanza walio wengi. Yale mawe ukiyaangalia yalivyokaa ndio utajua kuna nguvu kubwa inaulinnda ulimwengu na mabaya
Wachaga kama nitakuwa sahihi ni miongoni mwa makabila ya mwanzo kabisa kuendelea, sidhani kama kutakuwa na maeneo ya namna hiiHuko sidhan kama mazingira ya kuish ni magumu kiasi hicho kwan kiasi kikubwa huduma zote za kijamii zinapatikana
Aisee, kweli tembea uyaone. Hii inashangaza na kusikitishaKuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.
Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.
Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.
Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
Mkuu tusaidie jina la kijiji hii ni adventure aisee, nimecheka sanaKuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Respect hustler 🫡Maisha haya Mkuu, nilikuwa nawinda wanyamapori na kupasua mbao za mininga na Mikora huko. Operation tokomeza majangili ndio ilinikimbiza huko. Hivi yule Kombe alikuwaga na Duka la Dawa baridi yupo na duka lake lipo? Huko Ilunde sio mchezo miaka hiyo, kunasa kwenye mchanga ilikuwa ni kitu cha kawaida. Kuna kipindi tukikosa maji Porini ikabidi tuvue mashati yetu tulipofika sehemu kilipokuwa na tope, tukaweka tope na kuanza kulikamua via mashati yetu ili tupate maji. Salimia sana Zozzi Family, Kafirika, Mallack Family, Dotto Njeni hapo Mpanda.