Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni ile tu kwamba hujapazoea au ni mara yako ya kwanza. Je,unashtuka huku ni mara yako ya kwanza kufika. Na hapo, ni kufika na kuondoka. Tena unafikia senta kabisa. Waulize wanajeshi hali hizo ndo wanazijua sana.
Binafsi niliwahi kwenda Bunda,sehemu moja kuna kiwanda cha wahindi sijui cha pamba au mafuta. Masaa kama mawili tu! Mpaka wa leo sitamani kurudiko.
Au watu wanaojua Kigoma, sehemu moja mwaloni panaitwa Lubengela. Unapita Bulombola, mto malagarasi,unaenda weeeee! Unajiuliza watu walijuaje hapa! Ila kambi ya wavuvi,kwa aliepazoea,labda.
Kuna maisha ukiyaona au mazingira, na watu wanaishi fresh,unawaza kati ya msomi na asiesoma nani mjanja
 
Ruvuma.....Namtumbo.....Likuyu......huko kila penye pombe kuna uyoga( nyama ya tembo)...... pori kweli kweli.....Kuna mto Lumbegea...maji meupeeee
 
Ngoja nikumbuke vizuri jina la kijiji flani niliwahi kufika mwaka jana yaani kule watu bado wanajua rais ni Nyerere!
Kule ukisikia mtu anaongea kiswahili ujue ni mgeni hapo kijijini na wenyeji wakiona gari wanakimbia wanajua ni askari wanakuja kukamata wauza gongo na bange!
Hakuna barabara, hakuna umeme, mtandao wa simu haupo yaani ukifika kule ukiwa na smartphone watu wanaishangaa wanakuomba uwawekee movies watazame!
Maisha ni magumu sana hakuna maduka wala starehe yoyote zaidi ya kilabu cha pombe mwitu hasa gongo, ukame na njaa ndo mahala pake
Mademu wa kule wote wachafu wachafu akikatiza mbele yako unasikia harufu ya mnyama!
.mbaya zaidi kuna shule moja ya msingi waalimu wa hapo nao ni wapolipoli yaani wamefanana kabisa na mazingira ya huko mpaka wanaongea kiruga...kifupi niliondoka sijatafuna mbususu kabisa.
 
Tanzania hii ni kubwa sana nashangaa watu kujilinganisha na Rwanda, na Kenya kimaendeleo wakati hizo nchi zinaingia mara mbili kwa Tanzania
Tatizo statistics na calculation za kiuchumi haziangalii hivyo mkuu, ila kupitia uzi huu mimi mwenyewe nmekubali Tanzania ni kubwa balaa
 
Kijiji kingine ni mpyagula, kwa mbele kuna wasukuma wengi miaka ile wali na kambale mkubwa sana ilikua ni mia tano tu, mwenyeji wangu aliponiona kama nina mawazo akajadili na mke wake wakamwita binti mdogo wa mke wake aje anifariji chumbani na binti alikua mwanafunzi nilishangaa sana sitosahau hiko kisa
Dah, hiki kijiji cha kwenda kutembelea.
 
Kuna kijiji kipo katikati ya Kidete wilaya ya Kilosa na Mpwapwa magenge 30 kinaitwa Nana, kwa Mara ya kwanza nilikaa hapo wiki moja bila kuoga, dumu la maji ya mtoni ni buku mnatumia kupikia na kunywa, anayewauzia hayo maji akitoka alfajili kufuata maji na punda anarudi SAA 10 jioni.

Nilipoanza kutafiti maisha yao siku moja Mwenyeji akanipeleka kwa mama mmoja ndio ana club ya pombe za kienyeji ila Mimi nilikwenda kununuwa mihogo asubuhi tuchemshe kunywea chai kambini.

Sasa nikashangaa kila mlevi anayekuja pale amebeba kibegi cha sports mgongoni nikamuuliza mbona hii style siielewi? Akaniambia huku watu hawana pesa ukitaka kunywa pombe unakuja na maindi kwenye kibegi yanapimwa mama muuza anakupa pombe yeye anachukuwa mahindi, aisee Yale maisha ni Bonge la adventure kwangu.

Sehemu zenye madini zina asili ya kutokuwa na maji, madini na maji havikai pamoja, serikali iwahurumie watu hawa kuwapelekea maji maana hata ukichimba visima Mirefu huwezi kupata maji sehemu yenye madini.
Aisee, kweli tembea uyaone. Hii inashangaza na kusikitisha
 
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Mkuu tusaidie jina la kijiji hii ni adventure aisee, nimecheka sana
 
Maisha haya Mkuu, nilikuwa nawinda wanyamapori na kupasua mbao za mininga na Mikora huko. Operation tokomeza majangili ndio ilinikimbiza huko. Hivi yule Kombe alikuwaga na Duka la Dawa baridi yupo na duka lake lipo? Huko Ilunde sio mchezo miaka hiyo, kunasa kwenye mchanga ilikuwa ni kitu cha kawaida. Kuna kipindi tukikosa maji Porini ikabidi tuvue mashati yetu tulipofika sehemu kilipokuwa na tope, tukaweka tope na kuanza kulikamua via mashati yetu ili tupate maji. Salimia sana Zozzi Family, Kafirika, Mallack Family, Dotto Njeni hapo Mpanda.
Respect hustler 🫡
 
Back
Top Bottom