Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Niliwahi kwenda kijiji cha chabima kilosa morogoro ingawa kilikua na maendeleo kiasi pasipo na umeme wala mawasiliano kilichonishangaza nilikutana na mzungu mmoja yeye anaishi ndani ndani huko kajitenga mbali kabsa ana kambi yake na nyumba yake ya udongo. Anakula life tu. Kila ijumaa anawasha pikipiki yake na kwenda mjini kuchukua hela.

Nilimfanyia kazi flani ya juu kwa juu akanipa mpunga wangu nikasepa.
Pia kule ndio niliona kwa mara ya kwanza machine inalogwa haifanyi kazi😃...hv vijiji ukifika kuongea na wazee na kuheshmu mila zao muhimu sana... lasivyo hutamaliza kazi....
Kuloga sinema enzi izo acha bwana tabora Tanzania.

Yaani wanaroga jenereta watu wakiondoka linawaka
 
Kuna vijiji vinaitwa Chonwe na Udunghu vipo kata ya vidunda wilaya ya Kilosa Morogoro.

Sijui Sasa hivi ila miongo miwili iliyopita hakukuwa na barabara ya gari.

Unatembea kwa miguu ukipanda milima ila nilipenda hali ya hewa na wenyeji ni wavidunda walikuwa wakarimu sana. One day nitarudi kutembelea kata ya vidunda

Wavidunda oyeeh!
 
Vijiji vingi vya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu utashangaa wasukuma Sijui walifata nini huko, unakuta kijiji hakina umeme Wala maji. Yaan Maji yao wanachimba mabwawa kipindi cha mvua Maji yanatuama humo basi ng’ombe na binadam wote ndo mnakunywa Maji hayo!! Maji Kama maziwa kuna wachawi huko sijapata ona!! Wanga wananza kuwanga saa moja jioni!! [emoji2][emoji2]
Huko unakuta msukuma ana ng’ombe 50-100 ila anakula ugali na dagaa wa mwanza wale gredi ya mwisho kabisa ambao huwa kwaajili ya vyakula vya Kuku!![emoji2][emoji2] huko ikifika saa 12 jioni tembo kutoka serengeti wanaingia kijiji kula miwa[emoji23][emoji23]
🤣
 
Kijiji cha Ukumbikakoko, Kata ya Ukumbisiganga, Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora. Kwanza kabisa Kijiji hiki kipo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi, Wilaya ya Kaliua na Tanganyika. Shughuli Kuu ni uvuvi kupitia Mto Ugalla. Pia wakulima na wafugaji. Vinyumba vipo hapa na kuleeee kama mapengo ya mtoto. Kin entre ukitembea hatua ishirini umekimaliza, Shule ya Msingi Wanafunzi ni wakuwasehabu, ni kama ukoo mmoja tu. Njia Kuu ya mawasiliano ni reli ya Tabora to Mpanda. Wanakijiji wanazugia kilimo na uvuvi, lakini ni majangiri wa kufa mtu. Nyama ya porini unaelekezwa tu nenda nyumba ileee.
Huduma zote muhimu wanazichukulia Ugalla au Mpanda Mjini. Wanakijiji wajiona Land Cruiser Hard Top wote mbiooo, wanajua askari wanyamapori wamekuja kwenye masoko.
 
Habari za muda huu wana JF,

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya.

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji cha Baranga kata ya Sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndio kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu, jua kali ndio kwao, vurugu Sasa ndio chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa na mgogoro wa mpaka wa shamba kati ya ukoo na ukoo huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu nini?
Same sehemu za milimani!!!!
 
Wilaya ya Nachingwea kuna ka kijiji kanaitwa Mbondo, picha linaanza ikifika msimu wa mabibo tembo wanapishana kama malori barabarani.
Lakini watu wapo bwana No body cares na usalama wake.
Nilifika mwaka 2021 nikasema hiki kijiji sikanyagi tena.
 
Kijiji cha Ukumbikakoko, Kata ya Ukumbisiganga, Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora. Kwanza kabisa Kijiji hiki kipo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi, Wilaya ya Kaliua na Tanganyika. Shughuli Kuu ni uvuvi kupitia Mto Ugalla. Pia wakulima na wafugaji. Vinyumba vipo hapa na kuleeee kama mapengo ya mtoto. Kin entre ukitembea hatua ishirini umekimaliza, Shule ya Msingi Wanafunzi ni wakuwasehabu, ni kama ukoo mmoja tu. Njia Kuu ya mawasiliano ni reli ya Tabora to Mpanda. Wanakijiji wanazugia kilimo na uvuvi, lakini ni majangiri wa kufa mtu. Nyama ya porini unaelekezwa tu nenda nyumba ileee.
Huduma zote muhimu wanazichukulia Ugalla au Mpanda Mjini. Wanakijiji wajiona Land Cruiser Hard Top wote mbiooo, wanajua askari wanyamapori wamekuja kwenye masoko.
Kula nyama pori ni ujangili? Majangili ni wa Dp world mwananchi wa Tanzania kipaumbele nyama yetu hiwe nyama pori bucha kila sehemu
 
Back
Top Bottom