Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kuloga sinema enzi izo acha bwana tabora Tanzania.

Yaani wanaroga jenereta watu wakiondoka linawaka
 
Kuna vijiji vinaitwa Chonwe na Udunghu vipo kata ya vidunda wilaya ya Kilosa Morogoro.

Sijui Sasa hivi ila miongo miwili iliyopita hakukuwa na barabara ya gari.

Unatembea kwa miguu ukipanda milima ila nilipenda hali ya hewa na wenyeji ni wavidunda walikuwa wakarimu sana. One day nitarudi kutembelea kata ya vidunda

Wavidunda oyeeh!
 
🤣
 
Kijiji cha Ukumbikakoko, Kata ya Ukumbisiganga, Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora. Kwanza kabisa Kijiji hiki kipo mpakani mwa Mkoa wa Tabora na Katavi, Wilaya ya Kaliua na Tanganyika. Shughuli Kuu ni uvuvi kupitia Mto Ugalla. Pia wakulima na wafugaji. Vinyumba vipo hapa na kuleeee kama mapengo ya mtoto. Kin entre ukitembea hatua ishirini umekimaliza, Shule ya Msingi Wanafunzi ni wakuwasehabu, ni kama ukoo mmoja tu. Njia Kuu ya mawasiliano ni reli ya Tabora to Mpanda. Wanakijiji wanazugia kilimo na uvuvi, lakini ni majangiri wa kufa mtu. Nyama ya porini unaelekezwa tu nenda nyumba ileee.
Huduma zote muhimu wanazichukulia Ugalla au Mpanda Mjini. Wanakijiji wajiona Land Cruiser Hard Top wote mbiooo, wanajua askari wanyamapori wamekuja kwenye masoko.
 
Same sehemu za milimani!!!!
 
Wilaya ya Nachingwea kuna ka kijiji kanaitwa Mbondo, picha linaanza ikifika msimu wa mabibo tembo wanapishana kama malori barabarani.
Lakini watu wapo bwana No body cares na usalama wake.
Nilifika mwaka 2021 nikasema hiki kijiji sikanyagi tena.
 
Kula nyama pori ni ujangili? Majangili ni wa Dp world mwananchi wa Tanzania kipaumbele nyama yetu hiwe nyama pori bucha kila sehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…