Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.

Ertugul [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pia Kuna Kijiji Cha Msimba na Ng'apa pia Iyovi wilaya ya Kilosa- Morogoro watu wa kule sijui wanaishije maduka hamna Wala shule watoto wanatembe km 30 kufuata shule. Usiku Ni Giza tupu ukisafiri usiku hata usiku wa manane unakuta mtu Teena mwanamke Yuko barabarani na watoto wake wanatembe. Nyumba zao barabara hii wao hapa.
Ng'apa ipi?!!km ya Lindi sio kweli
 
Tabora Kuna sehem Moja Kuna njia panda ya kwenda mpanda na barabara lingine linaingia maporini......Picha linaanza mwenyeji alokuja kutupokea usiku mwenyewe alitupoteza, pili hatukua tukiona nyumba Wala chchte ni Giza tu......Tumesogea mbele tukashuka kweny gari kuangalia tuelekee usawa gani katokea bonge bonge ya joka tukakimbilia kweny gari tukaanza tena kuitafuta njia tukaipata

Tulivofika hapo msibani tukala tukala usiku nmelala nasikia kitu kikubwa kipo mgongoni kwangu kuwasha tochi nakutana na panya analinga a kichwa na Putin. Weeeh nlipiga kelele watu wote wakaamka nduki
Asubui nmeamka wakasema tuende tukapaone sehem alipozikwa ndugu yetu tukafika tukaanza kurudi nyumbani tukakutana tena na joka nlikua natetemeka hadi nikaingia period

Tukarudi nyumbani muda wote natembea sion nyumba za watu nkajiuliza Ina maan huku watu wanatokea wapi kumbe huko ndani ya msitu zaid

Siku tunarudi tukakutana barabarani na fisi mara na mbwa mwitu mara nyoka kakaa katikati ya barabara eeeh nyumba tukaona chache sana zenyewe ziko mbali mbali
Tulivofika center bwana weeeh nilijikuta nipo hospital maan nlikata moto gafla baada ya kusema tumbo linauma

Nilijiuliza watu huko wanaish vp, nyoka kila Kona, fisi mbwa mwitu,wanakunywa maji meupe kama maziwa, hospital ni mbali kias kwamba lazima uombe Pooh
[emoji3526][emoji38][emoji38][emoji38]km movie
 
Mkuu 😂😂😂
Mimi nina picha kabisa za hivyo vijiji nimefika huko yaani sehemu hata baskeli haifiki. Usafiri ni mitumbwi tu.
Niliwauliza hivi mnajua rais wa sasa hivi ni nani? Wakasema samia nikasema mmejuaje maana huku tv hamna wala network hashiki😂
Sema yale mazingira ya ziwani mazuri sana kama unataka kufanya retreat ya kujitenga na watu. Ukijani na ziwa + milima milima.
Yaani mtu anaamka asubuhi anaenda kupia mswaki ziwani maana ziwa lipo umbali kama wa mita mia.

Hiyo ya kulima milimani nilishagaa sana maana wakati wa kushukainabidi uwe makini kweli kweli unaweza kuteleza na kuanguka bondeni huko.

Baada ya kwenda hilo eneo niligundua kwanini Wasanii wakipanda kilimanjaro huishia njiai.
Mimi napenda nature, nimetembea mapori mengi humu TZ na kujionea mengi
Mgeni akienda uko analala wp boss kuna gesti?
 
Back
Top Bottom