Nimefanya kazi kama na kuishi huko. Nakushauri, nenda kapige mishe. Ni eneo zuri sana na watu wanalima sana. Kilimo kikubwa ni Mpunga na wanatoa kwenye bonde la Mwamapuli, Mamba, lake Rukwa na Kasansa. Kuna elimu za umwagiliaji za uhakika na Mpunga wanaolima hawatumii mbolea. Pana mzunguko mkubwa wa Pesa kwani wasukuma na Waha wengi wameinvest huko kwenye Kilimo, Biashara na ufugaji. Pia wanalima ufuta kama zao lingine la kibiashara. Pamechangamka sana na muda wataipata hadhi ya Mamlaka ya Mji mdogo Maji moto. Panapitika mwaka mzima kwa barabara za uhakika, unaweza kwenda Sumbawanga, Mpanda Mjini na Tabora pitia daraja la Kavuu. Nenda mkuu, ukiwa na akili unatoka kimaisha. Kunefunguka sana japo ni nilitoka huko 2014