Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Narudia tena hakuna mkoa masikini kama Dodoma.

Mkoa ule ni hatari huko wilayani.

Nilienda huko Kijiji Cha Chimendeli wilaya ya Bahi, Kwanza hiki Kijiji ndio kinaongoza kutoa omba omba wengi Sana tanzania.

Familia zinashindana kuja mijini kuomba omba. Mzazi anaweza kumtuma mtoto wake aende mjini awe omba au mzazi anaweza kuja mjini na familia nzima waje kuwa omba omba!

Kwa ambao mko Dar Es Salaam kuanzia Leo jitahidi ukikutana na omba omba watoto au wazee wadadisi Kwa maswali halafu waulize wanatoka Kijiji gani. Halafu piga nao story hutakaa uamini !


Kama ulivyo kwenu vijana wanasoma Kwa jihadi zote waje kuwa Madaktari Ila kuna sehemu hii tanzania watu Wana ndoto za kuwa omba omba. Au kama hamuamini Ulizieni hata walimu WA Shule walioko hicho Kijiji. Watoto hawaendi shule.

Sehemu ni kame.


Lile eneo unaweza kudhan upo Pakistan au Kule Yemen.


Eneo lingini ni vijiji vya wilaya ya kongwa.


Acha niishie hapa.
Dodoma mwish wa matatizo.huwa naona hat singida haina ukame kama ule wa dom.yan dodm kama ipo center
 
Nimefanya kazi kama na kuishi huko. Nakushauri, nenda kapige mishe. Ni eneo zuri sana na watu wanalima sana. Kilimo kikubwa ni Mpunga na wanatoa kwenye bonde la Mwamapuli, Mamba, lake Rukwa na Kasansa. Kuna elimu za umwagiliaji za uhakika na Mpunga wanaolima hawatumii mbolea. Pana mzunguko mkubwa wa Pesa kwani wasukuma na Waha wengi wameinvest huko kwenye Kilimo, Biashara na ufugaji. Pia wanalima ufuta kama zao lingine la kibiashara. Pamechangamka sana na muda wataipata hadhi ya Mamlaka ya Mji mdogo Maji moto. Panapitika mwaka mzima kwa barabara za uhakika, unaweza kwenda Sumbawanga, Mpanda Mjini na Tabora pitia daraja la Kavuu. Nenda mkuu, ukiwa na akili unatoka kimaisha. Kunefunguka sana japo ni nilitoka huko 2014
Kwa sasa ni zaidi.maji moto imeubgwa na lami ya kutoka tabora mpanda.ni lami tupu unaenda hata na vits bila waswas
 
sasa sehemu kama hiyo ndio njema sana kufika kwa wachaga unafika watu wamelala usingizi unachukua maeneo unajenga unafungua duka.Baada ya miaka mingi wakiamka wanatembea wewe ulishawaacha nyuma sana.
Hebu aise nipe contacts za hapo kwa urahisi kitu cha kwanza nafungua duka la kuuza mafuta ya taa,tambi za taa,maharage,mahindi,nitatoboa lazima
 
Kijiji cha mbagala kizuiani...jaman Kuna kunguni mpaka maji ya visima ukichota unakuta kunguni walidondokeamo.
Kunguni wanatembea msafara barabarani kama siafu
Wanalalaje maana hao jamaa hatar sana
 
Nilipanda mboga mashambani kwenda kuchuma nusura nibakwe na nyani...Sijui zilitaka kunipiga🤨 nilitimuka macho yote nilihamishia mgongoni😔
Ndio nisichokipenda linapokuja suala la ajira za umma..
 
Back
Top Bottom