Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Lakini mbona kuna watu wanatumia TV mbaya kabisa tena Sundar, TV za Sola na wamekaa nazo miaka mitano, halafu nyie mmeshindwa kukaa na Hisense miaka miwili tu. Hapo kuna mawili
1. Utunzaji m'bovu
2. Hiyo TV ulipigwa
Nyie ambao mnasema mmekaa na Hisense mwaka mmoja ikawaletea matatizo huwa siwaelewi, inawezekanaje kama sio mlipigwa kitu kizito na wauzaji wa Makumbusho [emoji1787][emoji1787]
Home kuna TV moja inaitwa Sundar ina miaka mwaka wa tano sasa haijawahi kusumbua chochote subwoofer zimeungua sana na hadi stabilizer ya umeme imungua fuse mara kwa mara lakini TV haijawahi kusumbua chochote ni nzima kama ilivyonunuliwa ishu ni utunzaji tu.
 
Wakuuu nishaurini Nichukue hii tv yenye specification hiziView attachment 2534077View attachment 2534078View attachment 2534079View attachment 2534080View attachment 2534081
Screenshot_20230301-210457_Chrome.jpg
 
Kwa kuzingatia haja yako ya kutaka kupata TV mpya ya 4K, hapa chini nimekuandalia orodha ya televisheni za 4K zenye ubora na bei nzuri kwa sasa nchini Tanzania.

#Brand na JinaMaelezoLinkBei wastani (TZS)
1LG UM7300Ina ukubwa wa inchi 55, teknolojia ya IPS 4K, inasaidia Dolby Vision na HDR10 Pro, na ina Smart TV yenye kiolesura cha LG webOS 4.5https://www.lg.com/eastafrica/tvs/lg-55UM7300PTA3,200,000
2Samsung RU7300Ina ukubwa wa inchi 65, teknolojia ya UHD Processor, inasaidia HDR10+ na HLG, na ina Smart TV yenye kiolesura cha Tizen OShttps://www.samsung.com/eastafrica/tvs/uhd-ru7300/UA65RU7300KXXA/4,500,000
3Sony X8000GIna ukubwa wa inchi 55, teknolojia ya 4K X-Reality Pro, inasaidia HDR10, HLG, na Dolby Vision, na ina Smart TV yenye kiolesura cha Android TVhttps://www.sony.co.tz/electronics/televisheni/x8000g-series3,700,000
4Hisense B7500Ina ukubwa wa inchi 50, teknolojia ya UHD Processor, inasaidia HDR10+, HLG, na Dolby Vision, na ina Smart TV yenye kiolesura cha VIDAA U 3.0https://www.hisense.co.tz/product/b7500/1,600,000
5TCL P715Ina ukubwa wa inchi 65, teknolojia ya 4K HDR Processor X1, inasaidia HDR10+ na HLG, na ina Smart TV yenye kiolesura cha Android TVhttps://www.tcl.com/tz/en/products/p715.html3,800,000
Natumaini orodha hii itakusaidia kupata TV ya 4K yenye ubora na bei nzuri. Unaweza kubofya link husika ili upate maelezo zaidi kuhusu kila TV na pia kuona bei halisi.
 
Kampuni zote mkuu inabidi uwe makini hata hisense ana vimeo vya kutosha tu.

Samsung TV zake za bei rahisi vioo vinatoka BOE (Mchina) hivyo unaweza nunua na ikawa na display mbaya vile vile.

Ila ikiwa Qled ama Oled uhakika huo sio mchina na hupati laki 6.

Nano tv ama hizi Qled nyingi ni kuanzia 1m kupanda, na Oled ni 3m kupanda.

Pia LED inategemea ikiwa na mwanga wa kutosha na standard nzuri kama Hdr10 inaweza kuwa nzuri pia ika compete na hizo Qled na Nano.
Mkuu, Model ipi ya Hisense you can recommend?
 
Mkuu punguza ujuaji, aliekwambia Samsung zote OG nani? Kwa zaidi ya 60% Tanzania tunatumia TV za Samsung fake, mwisho wa siku nunua kitu kulingana na uelewa wako lakini kikubwa uongozwe na budget yako

Mtu unakuta ana budget ambayo yeye alipenda kupata TV smart ya inch 43 ila budget yake hawezi kununua Lg, Samsung au Sony kwahiyo asinunue sasa? Uwepo wa makampuni mengi ya bidhaa lengo ni kila mtu apate kitu kulingana na uwezo wake

Ukitaka kujua tz tunapigwa sana we agiza TV China, Unaulizwa unataka Original?high copy au end copy? Na hapo hawamaanishi kwamba hizo copy na high copy zitaandikwa sumsung wala singsung bali zote ni Samsung unazikuta na kila kitu chake kama zilizo zingine

Samsung nchini kwetu nyingi sana zinakuja fake maana washajua kuwa tunapenda Jina ila uwezo wa kununua OG hatuna kwahiyo tunapewa kile ambacho tunaweza afford

Nenda posta Samsung store na model na series alafu omba uoneshwe TV original, we kazana uoneshwe TV original yani urudie tena unataka TV original, alafu icheki na chukua bei kisha Rudi kariakoo karinganishe bei

Hiyo ni option one, option 2 tafuta mtu alie China kisha mpe model ya TV ya Samsung aende Samsung store kisha apewe bei, na huko ndio atakutana na issue ya OG,High copy na end copy alafu usikie bei zao wenyewe uone kama tutaweza nunua

Usiishi Kwa kukariri mkuu, japokuwa Heshima ya Samsung kwenye ubora wa bidhaa zake kila mtu anaujua ila ukweli ni kwamba karibia zaidi ya 70% hawatumii Samsung OG kwa sasa ila wao hawajui tu

Walionunua TV za Samsung miaka ya zamani utagundua kuwa TV zao nyingi hadi leo zinadunda fresh tu, ila njoo Kwa hawa wanaonunua hii miaka ya karibuni ni kisanga Mzee mwenzangu

The same na kampuni zingine expensive kama vile Lg saizi tunapigwa tu kisa trade name, ata Hisense pia zina OG zake na fake zake, Tanzania hivi sasa kumejaa vitu fake, wakati iPhone 14 inatoka Yani china store hakuna ila teyari Tanzania kina bilnass wanaziuza na watu wananunua kama kawaida

Nenda posta au kariakoo Kwa mafundi wakubwa wa TV alafu ulizia ni kampuni gani Kwa sasa zinaongoza Kwa kufa, hadi mwaka Juzi me nipo kariakoo ilikuwa ni Samsung ikifatiwa na LG, Samsung ilikuwa inaongoza kufa kioo na LG ilikuwa inaongeza kuunguza AC

Nasema kariakoo na posta kwa sababu huko ndio walipo wanaotumia hizi kampuni, sio uende Kwa mafundi wetu wa kigogo au Manzese zimejaa TV kampuni za hadhi yao huwezi kuta hizo Samsung na lg wala Sony na ukikuta basi inatumika kama sampo tangu mwaka 2016, utakuta BOSS,Aborder,Zunne,singsung nk
Umeeleza vema kwa lugha rahisi sana,
 
Mkuu, Model ipi ya Hisense you can recommend?
Model zipo nyingi mkuu na zina Variety ndogo ndogo ngumu nikikwambia model fulani halafu ukaikuta. Cha muhimu ujue tu specs za Tv husika. Ukienda Dukani nenda na Simu halafu Google specs ujiridhishe.
 
Model zipo nyingi mkuu na zina Variety ndogo ndogo ngumu nikikwambia model fulani halafu ukaikuta. Cha muhimu ujue tu specs za Tv husika. Ukienda Dukani nenda na Simu halafu Google specs ujiridhishe.
Angetaja budget yake, anataka size gani, kipaumbele kwa TV yake ni matumizi ya kawaida au kucheza game etc.,, Sehemu atakayokuwa anaitumia kuna mwanga sana au la, hizi taarifa kidogo zingesaidia ku narrow down
 
Wadau nilikuwa na smart TV 4 K nchi 50 wale wajaa laana wakasepa nayo.

Nina Samsung Hd nchi 32 ilikuwa chumbani ndio nimeileta sebuleni yani tofauti ni kubwa sana.

Sasa nimeokota pochi la mzungu nataka ninunue TV ya kweli nirudi kwenye modern life.

Karibuni kwa ushauri.
Wazungu hawaweki hela ya maana kwenye pochi. Angalia vizuri hilo pochi lako, sanasana utakutana na business cards tu.
Kama hilo pochi lina hela kweli basi si la mzungu bali ni la Mwana CCM anayeenda kwenye uchaguzi au aliyetoka kusaini mkataba wa nchi
 
Model zipo nyingi mkuu na zina Variety ndogo ndogo ngumu nikikwambia model fulani halafu ukaikuta. Cha muhimu ujue tu specs za Tv husika. Ukienda Dukani nenda na Simu halafu Google specs ujiridhishe.
Ahsante sana mkuu
 
Angetaja budget yake, anataka size gani, kipaumbele kwa TV yake ni matumizi ya kawaida au kucheza game etc.,, Sehemu atakayokuwa anaitumia kuna mwanga sana au la, hizi taarifa kidogo zingesaidia ku narrow down
Matumizi yangu ya TV ni kuangalia mpira, Filamu, kusafu mtandaoni.

Sio mpenzi wa Games.
Ninapenda picha nzuri. TV walau 55"
 
Back
Top Bottom