Malaika wa Kifo
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 4,052
- 4,621
Mkuu, mimi nina akili timamu na mwenyewe anajua anadili na mtu wa aina gani,Mbona kama usha nasa mkuu? Ulipo kubali kupokea simu achilia mbali kufungua biashara ndio habari yako iliishia hapo
Mwanamke ukishazaa nae na kama unataka mwanao/wanao wakupende muheshimu, mfanye awe rafiki yako, wajibika kama Baba ili hata watoto wasipokuona yeye mwenyewe ndo awaambie hiki kawanunulia baba yenu
Sifa kuu ya mwanaume ni kutumia akili kudili na mwanamke, mwanamke ukishamjua udhaifu wake ulipo hatakusumbua
Huyu najua anachohitaji ni uwajibikaji kama mzazi mwenzie, hivyo na mimi nipo active kwa hili
Huwa akiniambia mtoto anahitaji kitu fulani, kama ni cha muhimu nanunua nampelekea ila kama hakina umuhimu nitaangalia mbadala wake ambacho kitakuwa na umuhimu nitanunua nitampelekea akiniuliza alichoniagiza namjibu "siku nyingine"
Hivyo hata nikiondoka namuacha akiwa na furaha kuona Baba nawajibika
Kuhusu ishu ya biashara ni kwa ajili ya watoto mkuu,
Mwanamke hana shughuri yoyote ya kufanya hivyo ikitokea leo nimekufa watoto wataishije?, nani atawahudumia? Vipi kuhusu kuwasomesha? Maana ye yupo yupo tu muda wote anashinda nyumbani hana shughuri yoyote inayomuingizia kipato, kuna kipindi nilimwambia apeleke watoto kwa shangazi yao ili yeye atafute shughuri ya kufanya, siku naonana nae namkuta mtu kakonda hadi nikamwonea huruma
Namuuliza vipi ananijibu anauza duka la mjomba wake lakini biashara hakuna hivyo mjomba wake kaamua kufunga duka na yeye kulala njaa ni kitu cha kawaida, akaniomba kwa kuwa hana kazi ya kufanya basi ni vyema akachukue watoto awalee niwe nawahudumia wakiwa kwake
Hivyo na ukizingatia sa hv ndo anaitafuta 30yrs akili imeshamkaa sawa hivyo hata nikimfungulia biashara kuiua itakuwa ni ngumu maana kushapitia msoto mkali, na nilimuuliza, "ulipokuwa na mimi ulikuwa una mwili na unapendeza sa hv vipi mbona umekongoroka ilhali ulikuwa umeolewa?"
Ananijibu kwa kifupi tu, "Em niache kwanza sitaki hata unikumbushe" akinijibu hivyo mi najikuta namsikitikia tu
Na nimeshamtahadharisha, nimemwambia kabisa nikikufungulia biashara ukiiua nachukua watoto kisha wewe upambane na hali yako
Kifupi ninachokifanya sasa ni kwenda na biti yake tu, akizinguwa na mimi nazinguwa
