Ni suala la muda tu kabla CCM hawajatuletea 'Magufuli' mwingine

BM alichimba biti "hakuma selikari sijui ya nani? hii ni selikari ya fisiemu"
Hapo alikuwa hapendi vile wanaita selikari ya Magufuli.
Lakini mbona hadi leo imebaki vile vile. Kila kitu serikali ya Samia, mama katoa hela etc.
Jambo likisha anzishwa na tena kama ni baya haliwezi kufa kirahisi.

Viongozi wameendelea kujikomba na kumsifia "Mama" kama walivyo fanya kwa Magufuli.
 
Kipindi cha Jakaya machawa walikuwa hawapo, Uchawa umeanzia kwa JPM.
Kazi ya machawa Ni kusifia/kutetea pasipostahili sifa/utetezi.

Sasa kwa hizi tozo, mfumuko wa bei, maisha magumu bila machawa labda Raisi ajiuzuru.
 
..hapana.

..matendo ya Magufuli hayakuwa yanaendana na mtu ambaye yuko karibu na anashauriwa na Ben Mkapa.

..Magufuli angekuwa anashauriwa na Mkala asingeharibu taswira ya nchi kimataifa na kidiplomasia kiasi kile.
Kwani kuna nchi gani ilitangaza kufunga ubarozi wake hapa Tanzania kisa uhusiano umearibika?

Zaidi tulirejesha ubarozi kwa Israel tu! Diplomasia ni pana sana na Diplomasia always ni ujasusi! Kwa bahati mbaya sana Africa tunachukulia Diplomasia kama sehemu za handshake kitu ambacho sio sahihi.
 
Ukiwauliza mbona hapo Kenya vyama ni vipya kila uchaguzi, na Kenya bado wako mbele yetu kwenye uchumi, afya, elimu, siasa nk wanapotezea.
Vyama ni wanachama ambao ni watu. Huo upya wa vyama unatoka wapi wakati kina Odinga ni walewale kila uchaguzi! Utasikia leo odm, kesho narc, kesho kutwa azimio...

Hivi chadema ingeshinda 2015 kuna mtu mwenye akili angetamba kwamba ccm imeondoshwa madarakani?
 
Kipindi cha Jakaya machawa walikuwa hawapo, Uchawa umeanzia kwa JPM.
Kazi ya machawa Ni kusifia/kutetea pasipostahili sifa/utetezi.

Sasa kwa hizi tozo, mfumuko wa bei, maisha magumu bila machawa labda Raisi ajiuzuru.
Swala la kusifia mi nililisia ata kwa Kikwete, suala Mh Jakaya katoe hela tujenge hikihiki na kile zilikuwepo sema tu 2014 huko ni mbali hukumbuki
 
Unakumbuka mabango ya kampeni mwaka 2015? % kubwa ya mabango ya kampeni 2015 yalikuwa na maneno chagua Magufuli, Hapa kazi tu sio Chagua CCM! Unajua kwanini? CCM 2015 ilikuwa hoi bini taaban,.
 
Wow! I like this man! Comment yake imenifurahisha Sana hasa hapo kwa Kenya. Vyama Ni vipya kila kukicha na mambo yanaenda.
 
Kwahiyo Republican wakiingia madarakani huko Marekani, huwa unaona ni democrat wako madarakani maana watu ni walewale? Hii ni logic ipi?
 
Alikuwa na mapungufu ila alikuwa na nia ya dhati ya kuona nchi inasonga mbele tofauti Sana na wale wahuni walioigeuza ikulu kuwa sehemu ya kuufanyia biashara na kulindana kwa msemo wa ''ccm ina wenyewe''
 
CCM yenye VISION ilikuwa ya Nyerere.

Baada ya sera za uchumi kushindwa na Nyerere kung'atuka mwaka 1985, CCM haijawahi kuwa na DIRA Tena.

Inachofanya na kung'ang'ania Madaraka huku ikiendelea KUJITAFUTA.

Na ukiangalia sasa hivi, mbinu wanayotumia Ni KULA na Kila mtu anayejifanya Ana influence kwenye JAMII kuanzia Vyama vya siasa, viongozi wa dini, wasanii, media, Vyama vya wafanyakazi, NGOs.

Akipataikana mtu Ana influence wanampa cheo.
 
Unakumbuka mabango ya kampeni mwaka 2015? % kubwa ya mabango ya kampeni 2015 yalikuwa na maneno chagua Magufuli, Hapa kazi tu sio Chagua CCM! Unajua kwanini? CCM 2015 ilikuwa hoi bini taaban,.

Kwani hata sasa CCM iko imara, au matumizi ya vyombo vya dola ndio uhai wake?
 
..hapana.

..matendo ya Magufuli hayakuwa yanaendana na mtu ambaye yuko karibu na anashauriwa na Ben Mkapa.

..Magufuli angekuwa anashauriwa na Mkala asingeharibu taswira ya nchi kimataifa na kidiplomasia kiasi kile.
JPM Aliharibuje taswira kimataifa? Kuna nchi tulikosana nayo? Kuna uhusiano tulivunja? Kifupi sema tu wazungu walikuwa hawampendi kwa sababu walishazoea kufaidi rasilimali zetu kwa Bei chee, JPM alikuwa na msimamo kitaifa kwa maslahi ya wengi.
Waliompinga wengi wao ni kwamba aliingilia maslahi yao waliyoyachuma kifusadi iwe kwenye CCM au serikali. Hawa ndiyo walitaka na wanaendelea kuaminisha baadhi ya watu kwamba Magu alikuwa ni katili (bila ushahidi) Mwengine anaweza kumpa jina baya kwa sababu aliondolewa kazini kwa vyeti feki. Kuna waliochota mali za CCM bila utaratibu, akiguswa, ooh Mwenyekiti mbabe.
Ukichanganya hao na jamaa zao lazima watamchukia, watapinga na kuchelewesha miradi kama SGR, MNHPP, ili waweze kuingia mikataba na kampuni wanazozijua ili zizalishe umeme mbadala, megawati 2,100 Au ndo kitengeneza ushindani wa kibiashara na MNHPP, naendelea kutafiti hilo.
Utasikia maiti ziliokotwa kwenye viroba. Juzi hapa nilisikia maiti ziliokotwa tena ila sijaona wanahabari wetu wakiendeleza hilo, yule Twaha kabana mdomo kimyaa!
RIP
 
Bado unaleta hadithi zile zile za kushtakiwa MIGA

Watu wanakunyonya kwenye mikataba ya uwekezaji alafu unaogopa kuwagusa kisa utashitakiwa na utaharibu taswira ya nchi..!??
Wewe pia nili Sukuma gang
 
Hahahahaha, mkuu ina maana wewe pekee ndiye hujui kuwa Jiwe alikuwa muuaji na muovu kuliko mtu yoyote Tanzanian?
 
Alikua na mapungufu yake mengi lkn ukweli ni kwamba alikua na nia njema kuona nchi ikisonga mbele.

Nilipenda sana jinsi alivokua akiwadhibiti wapuuzi waliojifanya hii nchi ni Mali yao na familia zao, tunahitaji rais mzalendo na asie yumbishwa na wahuni kwa kujifanya CCM ina wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…