JPM Aliharibuje taswira kimataifa? Kuna nchi tulikosana nayo? Kuna uhusiano tulivunja? Kifupi sema tu wazungu walikuwa hawampendi kwa sababu walishazoea kufaidi rasilimali zetu kwa Bei chee, JPM alikuwa na msimamo kitaifa kwa maslahi ya wengi.
Waliompinga wengi wao ni kwamba aliingilia maslahi yao waliyoyachuma kifusadi iwe kwenye CCM au serikali. Hawa ndiyo walitaka na wanaendelea kuaminisha baadhi ya watu kwamba Magu alikuwa ni katili (bila ushahidi) Mwengine anaweza kumpa jina baya kwa sababu aliondolewa kazini kwa vyeti feki. Kuna waliochota mali za CCM bila utaratibu, akiguswa, ooh Mwenyekiti mbabe.
Ukichanganya hao na jamaa zao lazima watamchukia, watapinga na kuchelewesha miradi kama SGR, MNHPP, ili waweze kuingia mikataba na kampuni wanazozijua ili zizalishe umeme mbadala, megawati 2,100 Au ndo kitengeneza ushindani wa kibiashara na MNHPP, naendelea kutafiti hilo.
Utasikia maiti ziliokotwa kwenye viroba. Juzi hapa nilisikia maiti ziliokotwa tena ila sijaona wanahabari wetu wakiendeleza hilo, yule Twaha kabana mdomo kimyaa!
RIP