Ni tabia gani umepanga/ulipanga kuiacha kufanya punde tu ukiuanza mwaka mpya? Vipi matokeo yake.

Unapokuwa unatamani kutumia soda , jitahidi utumie kununua maji kama mbadala hii mbinu niliitumia na nina miaka 8 sasa situmii soda.
 
Habari wakuu, herini wote kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tukiwa kwenye siku ya mwisho ya mwaka 2023 ni jambo jema sana kumshukuru Mungu na kumuomba atuvushe salama wote tuuone na kuuanza mwaka mpya wa 2024.

Kama ilivyo kawaida kwa miaka mingine iliyopita, baadhi yetu huweka maazimio ya kufanya kitu fulani kwa mara ya mwisho na kuahidi kubadilika kabisa mwaka mpya ukishaanza. Wengi ni ishu ya tabia na mazoea ya kufanya jambo fulani kwa mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kujichukulia sheria mkononi na tabia nyinginezo.

Hii ya kufanya kwa mara ya mwisho inawagharimu wengi sana na kushindwa kuacha tabia husika.

Binafsi mwisho wa mwaka jana niliweka azimio la kuachana na unywaji wa soda kabisa ila nimeshindwa kulifanikisha hilo, kwa kiasi fulani nimepunguza ila sijaweza kuacha jumla. Nipeni mbinu wakuu.

Ni tabia gani unapambana kuiacha kila mwaka na imeshindikana? Tupeane mbinu za kuacha/kuondokana kwa waliofanikiwa kuachana na mazoea/tabia hizo.

Wale wa kushindana na pombe na wanawake slow down ni hatari kwa afya.

Tuumalize mwaka 2023 salama wakuu.

NB: Pambana na yale mambo yaliyokukwamisha mwaka uliopita ufanye mwaka mpya kuwa wa kipekee kwako na wanaokuzunguka.
Marufuku kuwa na rafiki.
 
Kupunguza matumizi ya soda, hii limeshashindikana kwangu miaka mitatu najaribu lakn waaapi.......nkitoka nje ya dar naweza kaa wiki sijagusa ila nkirudi asubuhi na mapema tu walete Kati na Takeaway au sprite/mirinda niga/7up/ Pepsi baridi mchana, mara nyingi asubuh joto Kali nashindwa kunywa chai natumia sana soda

Npo rough sana kwenye matumizi ya pesa😢 najaribu kuandika mahesabu pembeni naanza jtatu....j4 ohooo huko mbele naandika maumivu, nkipanga langu nikatimiza kinachofuata Kuna fungu linaenda kuumia, nkikutana na marafiki tuliopotezana mda mrefu Kuna fungu linaenda umia, nikipata usajili mpya(elewa) fungu inaenda umia
 
Habari wakuu, herini wote kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tukiwa kwenye siku ya mwisho ya mwaka 2023 ni jambo jema sana kumshukuru Mungu na kumuomba atuvushe salama wote tuuone na kuuanza mwaka mpya wa 2024.

Kama ilivyo kawaida kwa miaka mingine iliyopita, baadhi yetu huweka maazimio ya kufanya kitu fulani kwa mara ya mwisho na kuahidi kubadilika kabisa mwaka mpya ukishaanza. Wengi ni ishu ya tabia na mazoea ya kufanya jambo fulani kwa mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kujichukulia sheria mkononi na tabia nyinginezo.

Hii ya kufanya kwa mara ya mwisho inawagharimu wengi sana na kushindwa kuacha tabia husika.

Binafsi mwisho wa mwaka jana niliweka azimio la kuachana na unywaji wa soda kabisa ila nimeshindwa kulifanikisha hilo, kwa kiasi fulani nimepunguza ila sijaweza kuacha jumla. Nipeni mbinu wakuu.

Ni tabia gani unapambana kuiacha kila mwaka na imeshindikana? Tupeane mbinu za kuacha/kuondokana kwa waliofanikiwa kuachana na mazoea/tabia hizo.

Wale wa kushindana na pombe na wanawake slow down ni hatari kwa afya.

Tuumalize mwaka 2023 salama wakuu.

NB: Pambana na yale mambo yaliyokukwamisha mwaka uliopita ufanye mwaka mpya kuwa wa kipekee kwako na wanaokuzunguka.
Kulala mapema yaani kulala saa tatu au nne kamili nimeshindwa lakini sijashindwa kabisa
 
Back
Top Bottom