Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulishawahi jaribu ukashindwa?Kuacha umbea na ufukunyukuu,
[emoji23][emoji23][emoji23] cjui km ntaweza.
Uza bodaboda ndio suluhishoNataka niache kula wake za watu na vitoto vya form four b jamani maana hii bodaboda yangu ndio chanzo cha hayo yote.
SiweziiiUlishawahi jaribu ukashindwa?
Ni kweli mkuu, mda utafika na nitaacha kabisa.Kidogo kidogo hujaza kibaba
Dah sema, walimwengu ndo wananikwamisha sana, sijui wananiroga 😟Habari wakuu, herini wote kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Tukiwa kwenye siku ya mwisho ya mwaka 2023 ni jambo jema sana kumshukuru Mungu na kumuomba atuvushe salama wote tuuone na kuuanza mwaka mpya wa 2024.
Kama ilivyo kawaida kwa miaka mingine iliyopita, baadhi yetu huweka maazimio ya kufanya kitu fulani kwa mara ya mwisho na kuahidi kubadilika kabisa mwaka mpya ukishaanza. Wengi ni ishu ya tabia na mazoea ya kufanya jambo fulani kwa mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kujichukulia sheria mkononi na tabia nyinginezo.
Hii ya kufanya kwa mara ya mwisho inawagharimu wengi sana na kushindwa kuacha tabia husika.
Binafsi mwisho wa mwaka jana niliweka azimio la kuachana na unywaji wa soda kabisa ila nimeshindwa kulifanikisha hilo, kwa kiasi fulani nimepunguza ila sijaweza kuacha jumla. Nipeni mbinu wakuu.
Ni tabia gani unapambana kuiacha kila mwaka na imeshindikana? Tupeane mbinu za kuacha/kuondokana kwa waliofanikiwa kuachana na mazoea/tabia hizo.
Wale wa kushindana na pombe na wanawake slow down ni hatari kwa afya.
Tuumalize mwaka 2023 salama wakuu.
NB: Pambana na yale mambo yaliyokukwamisha mwaka uliopita ufanye mwaka mpya kuwa wa kipekee kwako na wanaokuzunguka.
Umeandika point kubwa.Ukweli ni kwamba watu wanatakiwa wa~focus kwenye value ya 24hours, nikiwa na maana ya kuipa heshima EVERY SINGLE DAY.
Haya masuala ya kusibiri mwisho wa mwaka ndio mtu ubadilishe life style huwaga ni excitement tu ya kuuona mwaka mpya,na baada tu ya kupita siku mbili tatu unashangaa umejikuta umerudi kwenye cycle ya tabia ulizoazimia kuacha kama kawaida.
Watu tujifunze kuona thamani ya kila siku mpya
Hongera sana, mimi ntajizuia ila kuna muda nashindwa kabisa nakunywa.katika vitu niliacha kimasihara tu ni soda, na hapo home kulikuwa na sherehe tatu mfululizo, nakumbuka nilipewa soda nikajikuta tu nimesema situmiagi soda, mwaka wa 3 sijagusa soda na juice zoote za makopo.
Unaruhusu wafanye hvyo, usiruhusuDah sema, walimwengu ndo wananikwamisha sana, sijui wananiroga 😟
Uwezi au utaki?Siweziii