Ni tabia gani ya rafiki au mpenzi wako ilikushangaza mlipoanza kuishi pamoja?

Alikuwa anapenda usafi sana huyo.
 
Kwa muonekano wake(bibienu), Nilidhani asingekuwa anajua kupika

Nimekula vyakula kwa Wazazi, migahawani, hotelini n.k, lakini pale ndiyo mwisho wa reli

Nikikosa chakula chake, bora niagize kuku choma nile, nilale

Usihoji undani wa kitabu pasipo kuanza kufungua ukurasa wa kwanza 🙌
 

Kilichokuwa kinanikera ni kwamba ukishakula unataka kupumzika na kujiandaa kulala, lakini yeye anaanza kuhangaika kuosha vyombo. Nilikuwa nakereka sana kwa kweli!
Mi nilishangaa demu mmoja kila nikifanya jambo napewa pole,nikinyanyuka pole nikikaa pole ,yaani hadi nikiamka pole ,nikimaliza kula pole hadi nikipiga chafya pole .
Nikawa nashindwa kueleuwa ila kiukweli Sijui kama lile toleo la aina lile kama bado lipo.
 
Kwanini atake kuosha usiku mtu unataka kupumzika?

Akifanya asubuhi anapungukiwa nini?
Wewe ni aina ya wale watu wachafu wachafu tu sasa kama mwenzio anapenda usafi si u unajifunza kuanzia hapo?
 
Hapo kwenye vyombo mimi ndio naosha kabla sijalala hao warembo ndio wanashangaa
Hata nikiwa mwenyewe siwezi lala na vyombo vichafu ndani
 
Hapo kwenye vyombo mimi ndio naosha kabla sijalala hao warembo ndio wanashangaa
Hata nikiwa mwenyewe siwezi lala na vyombo vichafu ndani
Kuna nchi Africa Magharibi , wanaamini kulala au kuacha vyombo vichafu kunakaribisha roho chafu ndani.

Huyo dada ni mchafu tu mpaka anashangaa...mwenyewe nikitumia vyombo naviosha.
 
Wewe ni ke au me?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…