A
Anonymous
Guest
Waumini na Wanachama wa kwaya katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi, iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam tuna hoja ambayo baada ya kuwa chinichini tumeona bora ifike hadharani, Dunia ijue labda hatua zitachukuliwa.
Kuhusu ubadhirifu wa fedha
Ndani ya kwaya yetu ya Mtakatifu Monika ambayo imetimiza miaka 40, tulikuwa katika maandalizi ya kualika wadau na waumini ili tusherekea kutimia umri huo, uongozi wa kwaya ulipendekeza na kuandaa kadi za kuchangisha fedha.
Kitu kilichotushitua na kutusikitisha sana ni kwamba, hivi karibuni tuliambiwa kuwa fedha zote zilizochangwa na wadau kwa ajili ya jubilei yetu ya miaka 40 hazikuingia kwenye akaunti ya kwaya, bali zimeenda ndivyo sivyo!
Tumeelezwa kuwa fedha hizo zimepelekwa na kuingizwa kwenye akaunti binafsi ya mtu mmoja ambaye waumini na wanakwaya hata hawamjui! Hivi kweli jambo hili linaingia akilini?
Swali linabaki, kadi zilizosainiwa na kwenda kwa wadau ziliingizaje akaunti ya mtu binafsi? Wahusika wanadai kuna namba moja ilikosewa, je jina nalo lilikosewa?
Tunaamini Viongozi wanajua kabisa ni nani aliyechukua fedha hizo na ni kiasi gani kimechukuliwa, lakini cha kushangaza kiongozi wa kanisa anasita kuchukua hatua kali za kisheria!
Alipokwenda benki, waliandikiwa barua kuwa hii ni kesi ya polisi na inatakiwa ifuatiliwe kisheria ili watuhumiwa wawekwe ndani, lakini Paroko hataki kuwapeleka polisi akidai hataki kuwafunga wanaye!
Tunajiuliza kwa nini Mwenyekiti na Paroko wanazunguka badala ya kuchukua hatua madhubuti? Mmoja wa waliotenda madudu haya ni dereva wa Paroko mwenyewe, ambaye amekuwa hapo parokiani kwa miaka mingi na ndiye mwenyekiti wa kwaya! Yeye ndiye aliyewaletea karatasi na kumshawishi Paroko asaini bila kuhoji.
Baada ya sekeseke lote, Paroko akaamua kuisimamisha na kuizuia sherehe yetu, hivi sasa tunasubiri kupata majibu ya uwazi na yenye mashiko. Kama uongozi hautachukua hatua stahiki na kuweka mambo wazi, tupo tayari kuleta msukosuko na kuvua nguo uongozi huu hewani ili haki ipatikane na ukweli ujulikane!
Inasemekana akaunti hiyo ina uhusiano na mmoka kati ya watu wanaohusika na masuala ya kifedha, hivyo ni michezo ambayo tunachezewa ili tu watu wapige fedha.
Maadili kukiukwa
Kuna jambo lingine linaloendelea na uongozi wa Kanisa haujui, maadili yamevurugwa sana, kuna suala la ushoga linatajwa, kuna kiongozi mmoja wa kwaya anataka lifunikwe lisisemwe popote hata Viongozi wa Kanisa wasiambiwe.
Uongozi wa kanisa uliopita uliwahi kushughulikia changamoto ya aina hiyo, ambapo mhusika aliyetajwa alifukuzwa, kwa nini sasa hatua hazichukuliwi mapema.