Ni trilion ngapi zinatosha kujenga Hospitali inayokidhi matibabu ya viongozi wetu ili wasiende tena India? India imekuwa Jehanamu inameza viongozi we

Ni trilion ngapi zinatosha kujenga Hospitali inayokidhi matibabu ya viongozi wetu ili wasiende tena India? India imekuwa Jehanamu inameza viongozi we

Huu mtindo wa kwenda India umerudi kwa kasi ya ajabu.
Magufuli alidhibiti hii hali na walio kuwa wanapewa kibali ni wachache sana, kulikoni sasa tena.
Waziri wa Afya Mama Jenista Muhagama anapaswa adhibiti hii hali.
Magufuli alithibiti, halafu kilichofuata akafia Mzena Hospitali Kijitonyama
 
Mbona hizi zilizopo ziko standard za kimataifa kabisa, mfano Mloganzila, Muhimbiri, ilala Amana nk wawe wanapelekwa huko.
 
..Mloganzila inaweza kuwa hospitali ya Rufaa kwa viongozi wetu.

..Na imeshaanza kuwezeshwa. Kuna taarifa zilienea kuwa Mloganzila wameanza na huduma ya kuongeza makalio.
🤣

Sasa chief! Kuongeza makalio sio ugonjwa mkuu, ni ujinga
 
Ifahamike kwamba, inaeezekana kabisa kuwachukia viongozi wetu kwa baadhi ya mambo hasa ya kisiasa ila si kuona wala kusikia wakifa mara tu wanapougua na kwenda India kwa matibabu

Kama Taifa, kweli kabisa hatuna uwezo wa kujenga miundombinu bora na vifaa tiba vyote vinavyokidhi ubora kama India ambako viongozi wengi sasa wakiugua tu, utasikia wamepelekwa India kwenye matibabu

India sasa imekuwa kama Jehanamu inayomeza viongozi wetu

Kinazuwia nini sisi kujenga Hospital ya kisasa na vifaa tiba vya kisasa ili kuepuka kusafirishwa viongozi wetu kwenda India kisha kurudi maiti?

Ni nani mwenye uthubutu wa kufanya hili?

Viongozi wetu tunawapenda, ifike hatua na nyinyi mpendeke, vaeni uthubutu wa kuanzisha mambo magumu kwenye ubongo wetu, Magufuli alisema, Kila kitu tu aweza, kazi ni sisi kuamua
Ni Unyani tu,Apedomia
 
Imekuwa kawaida kila mmoja kukumbilia India
Naona wengi ni mkumbo tu
Yaani nina hela nisiende Germany nikimbilie India
Hao wanaoenda naona labda ni hatua za mwisho
Lakini mbona wanasema Muhimbili mpaka wanafunzi toka nje wanakuja kujifunza?
Au kugunga plaster tu

Hawa viongozi nao bogus wengi, yaani wanaacha hospital za maana wanaenda Apollo
 
We unaongea pumba sema wajenge hospital watu wote tutibiwe hapa sis watu wa haliyachini tunakufa kama kuku kwa sababu ya kukosa matibabu sahihi viongoz wanatumia kod zetu kutibiwa nje
 
Imekuwa kawaida kila mmoja kukumbilia India
Naona wengi ni mkumbo tu
Yaani nina hela nisiende Germany nikimbilie India
Hao wanaoenda naona labda ni hatua za mwisho
Lakini mbona wanasema Muhimbili mpaka wanafunzi toka nje wanakuja kujifunza?
Au kugunga plaster tu

Hawa viongozi nao bogus wengi, yaani wanaacha hospital za maana wanaenda Apollo

Apollo yenyewe sio Lele mama

Ndio best hospital in south Asia

Standard za Apollo ni za juu sana kwa gharama nafuu
 
Nilipata nafasi ya kufanya matibabu hospitali ya Appollo india, ukweli ni kuwa hakuna lisilowezekana. Ukweli bongo hatujawa serious tu
Mkuu, hongera mno kufanya kazi kwenye hospital ya kimataifa

Neno hakuna lisilowezekana, naamini umeleta utani kidogo Dr.
 
Back
Top Bottom