Ni trilion ngapi zinatosha kujenga Hospitali inayokidhi matibabu ya viongozi wetu ili wasiende tena India? India imekuwa Jehanamu inameza viongozi we

Shida sio mjengo tu, ishu iko hapa, madokta wetu wengi wamesoma hapa hapa bongo kwenye vyuo vyetu visivyo na ubora, ambsvyo alama za kufaulu zinuzwa kwa pesa au ngono, sasa viongozi wetu wanajua hili kwamba tuna madokta fake kila Kona, na ni yupo taysri kutibiwa na dokta aliyefoji matokeo?
Pale muhimbili, iliwahi kutokea, mgonjwa wa kichwa, kapasuliwa mguu, wa mguu kapasuliwa kichwa. ! Hata ungekuwa ni wewe upo taysri kuweka maisha yako na afya yako kwenye mikono ya *madokta" Wa mchongo kama hawa!
 
Miundombinu na vifaa is the least of our worries.

Hayo ni mambo ya pesa tu, bajeti. Tukijibana, tukiongea vizuri na watu, tunaweza kufanya.

Tatizo kubwa kabisa si miundombinu na vifaa.

Tatizo kubwa kabisa ni utamaduni.

Kuna cousin wangu mmoja alikuwa anasema, kitu chochote unachoweza kukimaliza kwa pesa tu si tatizo, hiyo ni gharama tu. Matatizo yenyewe huwezi kuyamaliza kwa pesa tu, yanataka kujipanga kiakili zaidi.

Kwa mfano, hata ukijenga hospitali nzuri sana, yenye vifaa vizuri sana, kama wafanyakazi wake wanapenda rushwa, hawaaminiki kutunza siri za faragha za mgonjwa, wanaweza hata kutumika kuwamaliza wagonjwa, unafikiri watu wataiamini hiyo hospitali?

Ukiwa na hospitali nzuri lakini huna maintenance culture, unafikiri itadumu?
 
Mmmmm india kwa miaka zaidi 50 sasa wako no 1 duniani....kwa hiyo huduma duniani......nchi masikini unataka uweke hospital.kwa viongozi wengine je ? Tupambane haki zetu bado watu hawajui mlo wa pili itakuwaje zaidi 60% umasikiniii mkubwaa
 
 
Kifo ni kifo tu. Waache hawa jamaa wanaojiita viongozi waendelee na usanii wao, eti CCM imejenga hospitali bora za kisasa halafu wenyewe wanatibiwa nje ya nchi tena kwa gharama ya nchi,halafu sisi wananchi wa vipato vya chini tunagharamia matibabu na hata ukifa maiti inatozwa gharama za matibabu. Wacha waendelee kufa huko huko.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…