Ni uamuzi upi tatizo CHADEMA wa MBOWE kuutaka uenyekiti tena, au ule wa LISU kuitosa nafasi ya umakamu mwenyekiti na kumendea uenyekiti taifa?

Na niwakumbushe tu wasio na kumbukumbu ya kuwa , bila Mwamba saa hizi Lissu angekuwa shimo la Tewa !
Msiojua nini maana ya shimo la Tewa ruksa ku google !
Halafu anakuja mpuuzi mmoja eti Mbowe ng''ong''ong''o
 
kupitia chadema hawezi tena kua kiongozi lakini pia kua mgombea urasi wa chadema, kwasabb wajumbe watakao mchagua mwenyekiti wa chama chao Taifa, ndiyo hao hao watakao muidhinisha mgombea urasi wa chama hicho 2025...

Akina Devota Minja mwenyekiti mpya wa kanda ya kati anashinda uchaguzi, Lisu akishuhudia, na mara baada ya uchaguzi Devota Minja anachukua gari kuja Dar, kumsindikiza mwenyekiti MBOWE kuchukua fomu, ni mambo yakufikirisha sana, kwamba Lisu anaungwa mkono na nani sasa?

Naunga mkono kwamba,
Lisu hata kama ataunda chama cha siasa hakitadumu na hakitakua na nguvu kabisa, labda kitakua ni chama cha wenye midomo tu kama yeye πŸ’
 
Ccm kuingilia mambo ya CDM kwa nia ovu
 
Nimewaza kama wewe...kama ka familia kadogo tu ka Chadema kamewashinda kuongoza wataweza kuliongoza taifa kweli??? Na mbowe anaonekana ni mroho na mlafi wa madaraka inaonekana wazi hata akipewa nchi anaweza geuka Museveni au Kagame
 
Nimewaza kama wewe...kama ka familia kadogo tu ka Chadema kamewashinda kuongoza wataweza kuliongoza taifa kweli??? Na mbowe anaonekana ni mroho na mlafi wa madaraka inaonekana wazi hata akipewa nchi anaweza geuka Museveni au Kagame
umejieleza vizuri sana na kwa ufupi mno gentleman tena kwa mantiki kweli..

na umehitimisha maelezo yako kwa logic yenye ujumbe mpana mno na maana kubwa zaidi πŸ’ͺπŸ‘Š
 
Ccm kuingilia mambo ya CDM kwa nia ovu
Gentleman,
mtaalamu muandamizi wa masuala ya siasa za vyama, naachaje kwa mfano kuchambua, kueleza na kufafanua mambo ya siasa za vyama kadiri inavyofaa kwa faida ya wadau?

ni ngumu sana, siwezi kuacha kuwajibika hata kidogo.

hata hivyo,
ni muhimu kama wadau wa jukwaa hili kujikita kwenye hoja zaidi kuliko kunyioshea vidole wachambuzi na wataalamu wa mambo haya πŸ’
 
Twende Lissu
Mbowe ameharibu CHADEMA
Na wakimtosa Lissu tunahamia Kwa Hashimu Rungwe Mzee wa ubwabwa
 
Mimi sioni tatizo kwa sababu wote wawili wamekuwa mara kadhaa wakituaminisha kwamba hawana mgogoro kati yao, na hakuna mpasuko ndani ya chama chao, ila wakakiri kwamba wanatofautiana tu misimamo, ambalo ni jambo la kawaida sana katika siasa. Ila naona kuna makundi mawili ndani ya chama chao - moja liko upande wa Mbowe, lingine upande wa Lissu. Kama wao wawili wako pamoja haya makundi watayaunganisha; kama wao wawili hawako pamoja haya makundi mawili yataongeza mgawanyiko wao, maana yamechanganya pia na uchochezi wa hisia na kuchukua neno moja out of context na kuonyesha as if lilitumika dhidi ya kiongozi mwingine. Kwa mfano, Mbowe alipoulizwa kuhusu kutumia pesa za chama kwa mambo yake binafsi, yeye alijibu kwamba ni mfanyabiashara wa ndani na nje, na wala "si mbangaizaji". Wanaomuunga mkono Tundu Lissu huko mtandao wa X naona wanavyolitumia neno "mbangaizaji" ni as if Mbowe alimwita kiongozi mwenzake "mbangaizaji" wakati si kweli. Kwa vile si kila mtu anayeweza kusoma kila post inawezekana kiongozi mwenzake akisoma hizo posts za namna hiyo inawezekana kabisa akafikiri kiongozi mwenzake kamwita "mbangaizaji". Kuna vijembe pia vinarushwa kutoka upande wa Mbowe kwenda kwa Lissu. Ushabiki au ufuasi wa viongozi wa aina hii ni bure kabisa! Yaani kugombea tu nafasi ya uongozi mtu mwingine kunifanye mimi nianze kurukwa na akili, na kuwa mchonganishi hivyo! Sijui watu wengine wakoje!
 
Na niwakumbushe tu wasio na kumbukumbu ya kuwa , bila Mwamba saa hizi Lissu angekuwa shimo la Tewa !
Msiojua nini maana ya shimo la Tewa ruksa ku google !
Halafu anakuja mpuuzi mmoja eti Mbowe ng''ong''ong''o


Mbowe kumuokoa Lissu asife malipo yake ni Lisu kutokugombea uenyekiti?
 
Na mbowe kama mbowe, yeye anajionaje kuwa monopoly kwa cheo hicho miaka na miaka. Issue ni ndogo tu kama Mbowe anataka kuendelea, basi hata mishale ya ccm kwamba imekaa madarakani muda mrefu haina maana tena, au kwamba katiba mpya ni ya zamani hilo litakuwa ni la uongo. Ndio maana watu wanasema, ya nini kuwatupia lawama kwamba chama cha ccm kimekaa madarakani muda mrefu ili hali hata mwenyekiti wenu ni hivyo hivyo.

Nkurunzinza full masinonda. Hilo ndilo ninaloliona kwamba watu hawataki mtu mmoja tu ndio awe kiongozi miaka zaidi ya 20 na wengine walale tu fofofo, hii ya kukaa tu kusubiria hadi 68 ina ukakasi sana kwa kweli. Hata dingi wa familia huwa anaanchia madaraka ya nyumba kijana wake akifikia miaka 18 tu, yeye hubaki kutoa muongozo na ushauri kidogo dogo akiona kwamba kijana wake anayumba. Ndio hivyo hivyo kwa mbowe pia.
 
Tofautisha Katiba ya nchi inasema nini kuhusu uongozi wa nchi, na katiba ya Chadema inasema nini kuhusu uongozi wa chama. Malengo ya nchi na malengo ya chama ni vitu viwili tofauti. Tundu Lissu alisema katiba ya Chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi wa juu wa chama hadi 2006 ilivyofanyiwa marekebisho, na kuandika katiba ya sasa ya chama, ambayo haina ukomo wa uongozi wa juu. Alisema msingi wa kuibadilisha katiba yao ulikuwa kwamba chama kilikuwa bado kichanga, na haikuwezekana kuwa na kubadilishana uongozi katika mazingira ya wakati huo, ambapo hata kupata tu wanachama ilikuwa kazi. Alisema pia kwamba, kwa sasa chama nimekua na kuna haja ya kubadilisha katiba yao ili iendane na mazingira ya sasa. Kumbuka kwamba haya Lissu kayasema tu mwezi huu, na hivi karibuni baada ya kutia nia ya kugombea, na alisema anapendekeza hivyo, na hata kwa wabunge wa viti maalumu ndani ya chama. Kwa kufuata katiba yao ya sasa Mbowe ana haki ya kugombea. Nje ya katiba yao, kuwa na hiyo 'consideration' ya kuwaachia wengine ni jambo jema, na linabaki kuwa uamuzi wake, lakini hapaswi kulaumiwa kwa kugombea to the extend kwamba Lissu apite bila kupingwa. Hivi ndivyo ninavyoweza kuchangia kwa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…