Ni ujuzi Gani ukijifunza unaweza kupata kazi mtandaoni nakukupatia kipato?

Ni ujuzi Gani ukijifunza unaweza kupata kazi mtandaoni nakukupatia kipato?

Wakuu najua jf hii ina watu wengi sana ebu tupeane michongo tutoane tongotongo.hivi ni ujuzi Gani ukijifunzia unaweza kufanya kazi kama remote hata kama ukiwa Tanzania job unafanya na unapata kipato Kwa njia ya mtandaoni?

Najua platform ni nyingi sana je ni Zipi? Wakuu ambao mko mambele au mnajua hizi mambo ebu tusanueni madogo zenu, hata nikiingiza dora 5 Kwa siku siyo mbaya kuliko kukaa tu.
Dalili za kupenda mtelezo.
 
Jifunze programming na hasa python. Hii ni programming language inayokua Kwa Kasi zaidi, jifunze basic Kisha specify maana python ni kubwa. Unaweza kuspecify kwenye AI, machine learning, data science, Computer vision, Robotics. Python inakufungulia milango ya career nyingi zinazolipa.

Au jifunze cyber security, kutokana na Ongezeko la matumizi ya AI , cyber security nayo inakua Kwa Kasi. Jifunze basic Kisha chagua specification. Pia unaweza kujifunza cloud technology aidha ya Amazon, azure hasa cloud Engineer career. Hii sio programming kivile ni kujifunza kutumia mofumo husika. Kwa sasa kila kitu ni cloud & server.
Python mbona ni Programming language ya Mda mrefu sana?
 
Wakuu najua jf hii ina watu wengi sana ebu tupeane michongo tutoane tongotongo.hivi ni ujuzi Gani ukijifunzia unaweza kufanya kazi kama remote hata kama ukiwa Tanzania job unafanya na unapata kipato Kwa njia ya mtandaoni?

Najua platform ni nyingi sana je ni Zipi? Wakuu ambao mko mambele au mnajua hizi mambo ebu tusanueni madogo zenu, hata nikiingiza dora 5 Kwa siku siyo mbaya kuliko kukaa tu.
Kuna ujuzi mwingi unaoweza kujifunza na ukafanya kazi mtandaoni ukiwa Tanzania. Muhimu ni kuchagua ujuzi mmoja, kuujua vizuri na kutengeneza portfolio.

Mifano mizuri ni:

  • Graphic Design
  • Video Editing
  • Digital Marketing
  • Web Development / Programming
  • Virtual Assistant
  • Data Analysis
  • Content Writing & Copywriting
  • UI/UX Design
  • Social Media Management

Kwa anayeanza, ningeshauri Video Editing, Graphic Design au Virtual Assistant, kwa sababu unaweza kuanza kujifunza kwa vifaa ulivyonavyo na kujenga uzoefu taratibu.

Platform kama Upwork, Fiverr na LinkedIn zinaweza kukusaidia kupata wateja. Ila ukweli ni kwamba, siyo kujifunza leo halafu kesho pesa ianze kutoka; ujue skill, tengeneza portfolio, jifunze kutafuta wateja na uwe consistent.

Dola 5 kwa siku inawezekana, na inaweza kuwa mwanzo wa kitu kikubwa. Usitafute shortcut, tafuta skill inayouzwa.
 
Mkuu Nafaka kama hutojali unieleweshe hii AI data collection and training ni nini haswa na nikitaka jifunza naanzia wapi na kazi zake zinapatikanaje
Mkuu AI inakuwa trained na data za aina mbalimbali kutokana na hiyo model inalenga kufanya nini. Mfano: kuna data ambazo zinakuwa annotated... Ndiyo maana kuna kazi mtandaoni za data annotation. Yani ili AI iweze kutambua vitu kwenye picha, zinachukulia picha na kuzizungushia labda squares na kuiambia huyu ni paka, huu ni mti, huyu binadamu. Yani inafanyika kwa millions of pictures. Kuna data labda za kuifunza kutranscribe, kuzungumza n.k hizo zinakuwa za sauti na maandishi. So, kwa client wangu huyu, data tunazotumia ni Za sauti na maandishi. Tunaziscrap kutoka vyanzo mbalimbali zinakuwa in pairs. Lugha moja kingereza lugha ya pili ya kibantu. Zinakuwa arranges in sets kwenye spread sheet yani sentence moja moja kwenye kila row. Za sauti hizo approach ilikuwa ni kurekodi sentence milion moja na nusu.
Kwa sasa tayari runa models na APIs na nadhani client kama watatu. Kinachoendelea ni kuziboresha tu.
Wapo utapata kazi? Kazi hasa za annotation na data collection ni nyingi mtandaoni. Sema mara nyingi hazina pesa nyingi maana makampuni ya kihindi yamezichukua ni walanguzi. Hizi kazi naona one forma ndio wanazo zaidi na lionbridge. Ikiwa utapata kaa lionbridge utapata ela nyingi mnoo
 
Hyrax mi nishaingia tamaa huku, mwaka mzima umekata wacha nikatoe😎
 

Attachments

  • 87AA2CFD-5066-4900-817C-2A57A458A54D.jpeg
    87AA2CFD-5066-4900-817C-2A57A458A54D.jpeg
    267.3 KB · Views: 13
Back
Top Bottom