Bwana Simplemind, habari kwanza. Kupitia reaction yako, naomba nitoe wito kwa wa Tanzania tujaribu kwa na tabia ya udadisi na kujifunza. Pale tusipofahamu tukiri kwamba hatujui ili tupewe taarifa sahihi, na hilo ndilo ongezeko la ufahamu na maarifa. Mimi na umri wangu huu nakaribia miaka mia, sijawahi kumwona ila namskia kiumbe aitwaye nguva na hadith zake nyingi, mara ukiwa ziwani akatokea, akakugusa unapotea naye... n.k.
Kwa picha hii, ninategemea tutaulizana maswali mengi, tutafute source ya info hii, tuchanganue hoja ndipo tufikie conclusions. Sas vijana kubisha tu ni utapeli bila kutafuta facts, nina wasi wasi tutaendeleza kuimarisha utamaduni uliojengeka siku za hivi karibuni za kujadili bila hoja zaidi ya kufokeana na kutukanana tu na mwenye matusi mengi anaonekana kushinda.
There is always power in information. Tafuta taarifa sahihi kwanza uelewe ndipo uamue. Hujui kitu sema sijui na wala kutokujua jambo ni ujinga ambao si kosa. Ujinga unaimarika zaidi kwa ubishi na kutokutaka kutafuta taarifa sahihi za kuuondoa
Twende kazini