Ni upi umri sahihi wa kuacha kumuadhibu mtoto?

nimekupata vizuri
hapo kwenye ngumi weee hapana atahama kwa mda
Sasa utamhamishaje ukimwambia Hama anakupa makonzi inabidi ukae kimya yeye anageuka baba mwenye nyumba 😃😃 Kuna mstoto manunda mzee acha kabisa.
 
Kumuadhibu mtoto maana yake hujamlea kwa usahiihi kuna sehemu ulikosea kama mzazi.

Fimbo haimfanyi mtoto kuepukana na kosa kwa kujua madhara yake,bali fimbo inamfanya mtoto kuepuka kosa kwa kuhofia kupigwa,kwa maana akishajihakikishia kwamba hayupo katika maeneo ambayo akifanya kosa atapigwa basi ndipo huanza kufanya kwa vifichoo makosa hayo
Hongera sana mkuu.

Kuna watu walikuwa wananishangaa kwa nini nikiongea na mdogo wangu naongea naye kana kwamba yeye ni mtu mzima wakati yeye ni mtoto nimemzidi miaka mingi,hawakujua kwa nini.

Nilimfundisha sana madhara ya kila jambo kwa hoja na sio kwa kumkaririsha kwamba jambo hili mwiko huku akiwa hajui sababu hasa kwa nini halifai.

Mpaka hivi leo amekuwa ni kijana ambaye anajisimamia katika mambo mengi sana tofauti na vijana wengine kabisa,lakini hayo ni matendo ya kukaa nae kwa ustaarabu na kumuelekeza maisha yalivyo.

Kuna siku huyu dogo aliiba pesa sehemu wakati yuko mtoto,nikasema nakaa naye chini nikaanza kumuelekeza madhara ya wizi kwa upole sana kana kwamba sio yeye ambaye aliiba,nilimpa maneno ya kugonga nyoyo na kumuonesha kwamba sisi hatujaathirika kitu kwa yeye kuiba na wala haituumi ila tunamuonea huruma yeye kwa kuiba kwa sababu ndio ameanza kuingiza tabia mbovu rohoni mwake jivyo yeye ndio atakayepoteza sio sisi aliotuibia,baada ya kukaa naye siku kadhaa na kumpa maneno ya kistaarabu yule dogo aliacha kabisa wizi mpaka hivi leo.
 
Sasa utamhamishaje ukimwambia Hama anakupa makonzi inabidi ukae kimya yeye anageuka baba mwenye nyumba [emoji2][emoji2] Kuna mstoto manunda mzee acha kabisa.
[emoji1787][emoji1787]huyo atakuwa wa kusingiziwa sio bure aisee
 
Hongera kwa kufanikisha hilo mkuu upo vizuri
 
wazazi wanawafumania watoto wao wa kike umri wa miaka 10+ wanafanya mapenzi nyumban
Mtoto wa kike kavusha Mwanaume nyumban kwa mzazi
Unakutana na ushauri usimpige wewe muelekeze huyo mtoto
Mambo ya kuelekeza unataka kutengeneza mtoto aina ya Junior. Mtoto wa kiafrica wazazi wanamlea kizungu
 
Mweeeeh! Mtoto niliyemkojoa mwenyewe...
Labda niwe mgonjwa wa kupooza , wazazi wengine na sie tumekua kimafia.
Sometimes huwa natamani kujenga ka mahabusu hapa nyumbani.
Mimi napenda mtoto mwenye nidhamu kama jeshini.
Nachoshukuru wanangu ni marafiki zangu, naomba kwa Mungu anipe umri mrefu ili nihakikishe wanakuwa salama hadi hapo watakaposimama wenyewe kimaisha.

Mtoto akupige ngumi na awe mtawala home?
 
[emoji1787][emoji1787]
 
we noma kagereza kadogo
 
Kama anavutia kupiga na kama umefika ile hatua ya kupiga ngumi, mitama na mawe basi endelea kutembeza kipigo mpaka atakapohama hapo bomani kwako.
 
we noma kagereza kadogo
Si unajua watoto wanavyopenda michezo na kuwa free,sasa ukimpiga mahabusu ya 24 hrs lazima awe mpole.
Ila huwa nahofia wasije kukimbia hapa nyumbani[emoji3][emoji3]
 
Hahahah jamaa utaua😃😃
 
Si unajua watoto wanavyopenda michezo na kuwa free,sasa ukimpiga mahabusu ya 24 hrs lazima awe mpole.
Ila huwa nahofia wasije kukimbia hapa nyumbani[emoji3][emoji3]
[emoji1787][emoji1787]wangejihamisha wenyewe
 
Sheria ya kiislamu ni hadi miaka 15., kuanzia hapo tena mtoto anatakiwa kwa vyovyote afahamu jambo baya na jema, na mzazi kuanzia umri huo lile jukum la kumbana kimaadili na kumfundisha linaanza kuondoka kwenye dhamana yake., na mtoto anatakiwa aanze kuchapwa chapwa kwenye miaka 7 na kuendelea afunzwe ibada kidogo dogo hadi kufikia hapo 15 tena otherwise mzazi atakuwa na dhima kubwa juu ya mtoto kwa Mola wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…