Ni upi umri sahihi wa kuacha kumuadhibu mtoto?

Kabla hatujafika kwenye umri sahihi wa kuacha kumpiga mtoto. Tukubaliane kwanza mtoto hatakiwi kupigwa katika umri wowote, afu topic ikarest in pisi kali.
 
Wenzetu naona mwatuletea malezi ya kiulayaulaya hapa! Waafrika tuna mila na desturi zetu katika malezi, lakini hata maandiko kwenye waumini wa Kikristu ni kwamba usimnyime mtoto kiboko katika malezi, sasa ukisema umwelekeze na akagoma kuelekezwa umnunulie pipi na biscuits kumshawishi?!
 
saiv nina nganyoni anakula stiki za kutosha nikipata ndito naye hivyo hivyo suala la kuongea na mtoto nawaachia kina baba junior ,,,,,,ukikaa kwenye mstari ninaoutaka utakuwa rafiki yangu rather than that stick tuu mpka siku ninayo kusend off(wakike ) au harusi(wakiume)
 
Mtoto kufika tu miaka 17-18 anakuwa anarekebishika kwa kuongea nae tu kwa kumkalisha chini, kama atakuwa haelewi basi ndo imekula kwako hivyo... Hutoweza tena hata utumie nini, labda neema ya Mungu tu impitie.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante kwa kushare nasi
 
kwa maana hiyo kwako wewe hakuna mwisho full kumdunda tu kwa kuwa ni mtt wako [emoji848][emoji848]
 
Duh
 
miaka 17 hadi 18 [emoji848][emoji848]
 
Ukiona unaweza Kupigana nae we mpige tu ila ukiona kafikia umri wa kukutoa manundu kwa knockout ndo uache
 
Ukiona unaweza Kupigana nae we mpige tu ila ukiona kafikia umri wa kukutoa manundu kwa knockout ndo uache
kama ukiwa una mmudu hata kama kaoa au kuolewa[emoji848][emoji848]
 
Usimwadhibu kabisa, tangu mdogo (anapoanza kuelewa) uwe unaongea nae, unamweleza kwanini asifanye hivyo madhara yake. Usimwadhibu.

Wewe unaongelea watoto wa kizungu. Mtoa mada anaongelea mtoto wa Kiswahili/kitanzania
 
Wewe unaongelea watoto wa kizungu. Mtoa mada anaongelea mtoto wa Kiswahili/kitanzania
kabisa kwa mazingira yetu haya ya kibongo bongo na uzoefu wa malezi ya hapa kwetu maana ndimo tunapoishi
 
Sema umri wa mtt kuacha kuadhibiwa.
 
Kama amelelewa karibu na danguro unategemea nini? hizo ndio faida zake sasa.
Mtoto anajifunza kutoka kwenye mazingira na jamii ukiwemo wewe mzazi, sasa kama mazingira ni mabovu na wewe mzazi ndio vilevile basi tegemea kutengeneza time bomb.

Mtoto wa miaka 10 kuanza tabia mbovu ni kielelezo kwamba wazazi na jamii nzima hawajitambui na sio sababu alikuwa hapigwi.
Huyo mtoto hata upige kama punda hatosikia.
 
na hapa ndipo wahenga wanakuja sasa Samaki mkunje angali mbichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…