Ni ushamba sana kutoka semina umebebelea kopo la maji uliyopewa kwenye semina, warsha nk

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,113
Reaction score
6,251
Peace be upon you all,

Aise waTanzania ni watu washamba sana sana kabisa. Mwanzo nilidhani ni watumishi pekee wenye huu ushamba ila nimebaini ni watu wengi wa sekta zote.

Yani unakuta watu wamekwenda semina fulani alafu muda wa kutoka wamebebelea vimaji vya mia tano hako kakopo atakabeba njia nzima. Unajiuliza huyu ameshindwa kuyamaliza hayo maji na mara nyingi semina na warsha wanagawa vimaji vya 600 ml. (Vile vimaji vya 500 Tsh).

Wanamake sasa aise hawa ndugu ni washamba haswa, unakuta mmama na heshima zake semina imekwisha anaenda anaomba maji yaliyobaki chupa mbili tatu huyo anabebelea mpaka nyumbani, kwamba nyumbani kwake hakuna maji ya kunywa?

Na wenye ulimbukeni huu ni watu "wasomi" aise hopeless uncivilised graduates. Alafu wakiwa wamebebelea ukiwatazama hua wanaona fahari kweli kweli kutembea na maji waliyogaiwa kwenye semina, warsha nk
 
Wewe tusibebe maji? Tukipata kiu njiani? Yaani natoka sehemu ambayo nnaweza kubeba maji eti nisibebe kisa ushamba, nikifika njiani nitoe hela ninunue 😅😅😅😅labda sio mimi hayo ni maji tu ukikutana na wabeba pilau 😅
 
Kama mtu hajavaa jezi ya Yanga au shati la CCM ukikutana naye amebeba maji unafahamu vipi ni ya semina mkuu.
 
Una hakika maji yote wanayobeba huwa wametoa kwenye semina,wewe unapata shida gani watu wakibeba maji hata kama wamepewa,ujanja kwako ni kumaliza hata kama mwili hauna utaratibu huo,la mwisho fuata maisha yako binafsi hayo mengine waachie wenyewe na utapunguza kuuchosha ubongo wako wa kb 12
 
Wewe tusibebe maji? Tukipata kiu njiani? Yaani natoka sehemu ambayo nnaweza kubeba maji eti nisibebe kisa ushamba, nikifika njiani nitoe hela ninunue 😅😅😅😅labda sio mimi hayo ni maji tu ukikutana na wabeba pilau 😅
Aise umenikumbusha wengine wanabeba pilau minofu ya nyama kwenye mikoba, jamani huko nyumbani hakuna chakula.

Unakuta dada mzuri anatembea nzia nzima ananukia pilau, kumbe kwenye mkoba kafungasha pilau la semina.
 
Si bure... Mtoa mada itakuwa amenyimwa maji huyu...

Binafsi hata chakula nabeba vizuri tu, maana kwenye pochi yangu sikosi mifuko miwili au mitatu.
Njoo uniseme nipo hapaaa town kwenu
 
Sioni kama kuna ushamba hapo , ndio maan lile kopo unaruhisiw kubeba mkuu , cjui mantik yako imejikta wap
 
Peace be upon you all,

Aise waTanzania ni watu washamba sana sana kabisa. Mwanzo nilidhani ni watumishi pekee wenye huu ushamba ila nimebaini ni watu wengi wa sekta zote.

Yani unakuta watu wamekwenda semina fulani alafu muda wa kutoka wamebebelea vimaji vya mia tano hako kakopo atakabeba njia nzima. Unajiuliza huyu ameshindwa kuyamaliza hayo maji na mara nyingi semina na warsha wanagawa vimaji vya 600 ml. (Vile vimaji vya 500 Tsh).

Wanamake sasa aise hawa ndugu ni washamba haswa, unakuta mmama na heshima zake semina imekwisha anaenda anaomba maji yaliyobaki chupa mbili tatu huyo anabebelea mpaka nyumbani, kwamba nyumbani kwake hakuna maji ya kunywa?

Na wenye ulimbukeni huu ni watu "wasomi" aise hopeless uncivilised graduates. Alafu wakiwa wamebebelea ukiwatazama hua wanaona fahari kweli kweli kutembea na maji waliyogaiwa kwenye semina, warsha nk
Siku hizi Kuna mgawo wa maji ,hatari.
 
Back
Top Bottom