Ni ushamba sana kutoka semina umebebelea kopo la maji uliyopewa kwenye semina, warsha nk

Ni ushamba sana kutoka semina umebebelea kopo la maji uliyopewa kwenye semina, warsha nk

Peace be upon you all,

Aise waTanzania ni watu washamba sana sana kabisa. Mwanzo nilidhani ni watumishi pekee wenye huu ushamba ila nimebaini ni watu wengi wa sekta zote.

Yani unakuta watu wamekwenda semina fulani alafu muda wa kutoka wamebebelea vimaji vya mia tano hako kakopo atakabeba njia nzima. Unajiuliza huyu ameshindwa kuyamaliza hayo maji na mara nyingi semina na warsha wanagawa vimaji vya 600 ml. (Vile vimaji vya 500 Tsh).

Wanamake sasa aise hawa ndugu ni washamba haswa, unakuta mmama na heshima zake semina imekwisha anaenda anaomba maji yaliyobaki chupa mbili tatu huyo anabebelea mpaka nyumbani, kwamba nyumbani kwake hakuna maji ya kunywa?

Na wenye ulimbukeni huu ni watu "wasomi" aise hopeless uncivilised graduates. Alafu wakiwa wamebebelea ukiwatazama hua wanaona fahari kweli kweli kutembea na maji waliyogaiwa kwenye semina, warsha nk
Graduates walikufanya nini?
 
Sioni kama kuna ushamba hapo , ndio maan lile kopo unaruhisiw kubeba mkuu , cjui mantik yako imejikta wap
Mtoa mada ndo mshamba. Anadhani ufahari ni kuacha maji nusu yamwage halafu ukitoka nje ununue mengine.

Huyu jamaa atakwambia hata kubeba chakula kutoka nyumbani kwenda nacho kazini kwa ajili ya breakfast na lunch ni ushamba.

Huyu atakwambia kutembea kwa miguu kwenda kazi au kurudi kazini ni ushamba.

Huyu jamaa atakwambia kubeba mfuko wa kubebea vitu ukininia dukani ni ushamba. Yeye anataka kila ulinunua kitu ununue na mfuko.

Nawafahamu watu wenye mawazo kama huyu jamaa. Wanajionaga wao ni bab kubwa wakati hawana kitu. Wana tabia za ku show-off halafu mwisho wa siku wana strugle sana kwenye maisha na kufa wakiwa masikini.
 
Hujawahi kutana na wabeba visandarusi vya pilau wewe.
Hebu tupishe
 
Mtoa mada ndo mshamba. Anadhani ufahari ni kuacha maji nusu yamwage halafu ukitoka nje ununue mengine.

Huyu jamaa atakwambia hata kubeba chakula kutoka nyumbani kwenda nacho kazini kwa ajili ya breakfast na lunch ni ushamba.

Huyu atakwambia kutembea kwa miguu kwenda kazi au kurudi kazini ni ushamba.

Huyu jamaa atakwambia kubeba mfuko wa kubebea vitu ukininia dukani ni ushamba. Yeye anataka kila ulinunua kitu ununue na mfuko.

Nawafahamu watu wenye mawazo kama huyu jamaa. Wanajionaga wao ni bab kubwa wakati hawana kitu. Wana tabia za ku show-off halafu mwisho wa siku wana strugle sana kwenye maisha na kufa wakiwa masikini.
Kuna ndugu yangu mmoja alikuwa hataki tuchume mchicha tuliootesha nyumbani, ukipikq huo hali...
Anataka muende sokoni kununua. Aina ya mchicha ni ile ile.
 
Kwa nini tubebe maji baada ya semina kuisha?
1. Kunywa maji mengi na vinywaji vingine wakati wa semina kunaweza kukakuondolea utulivu wakati semina ikiendelea haja ndogo za hapa na pale haziishi.
2. Sio vizuri kunywa maji au vinywaji mara kwa mara ukiwa semina hiyo inaweza kukufanya ukaonekana kama sio mtulivu.
3. Kuondoka na maji kunaweza kukufanya ukabana bajeti ya kununua maji mengine njiani hivyo utasevu kiasi fulani.
4. Halafu yale maji ni yako tu hujapangiwa muda wa kunywa ila zingatia upo wapi na nani na mnafanya nini.
 
Back
Top Bottom