Ni ushamba sana kutoka semina umebebelea kopo la maji uliyopewa kwenye semina, warsha nk

Kuna binadamu mna roho mbaya sasa unataka maji yake amuachie nani kama hajayamaliza?

Mtoa post Acha makasiriko.
 
Huyo ni mimi kabsaaaa

iwe nimetoka kwenye semina au la, kama sina begi kubwa, lazma nitashikilia chupa ya maji mkononi kama bado nipo kwenye mizunguko yangu na sijali 📌📌
 
Hivi vitoto vya JF vinaleta thread kama hii ijadiliwe kweli??? huyu ndio great thinker???
nashangaa sana kuna kamoja juzi kalisema ati mtu kuongea kilugha chake ni ushamba . sijui mtu mshamba ni yupi?
mtu anatoka semina saa 10 jua limezama na anakwenda mbali... aache kubeba maji ili mvaa vinjunga na vi hereni asimuone mshamba?
 
Tunafanya maisha kuwa magumu kwa kupenda kufatilia na kutilia maanani vtu vidogo vidogo, Sasa mkuu niache maji halafu nikifika hapo mbele tu kidogo nikisikia kiu nianze tena kutafuta yanakouzwa ninunue?

Wengine muda wote tunatembea na maji iwe mkononi au kwenye begi.
 
sasa maji yamebaki unataka yarudishwe dukani?
 
wewe ndio Mshamba sana, nakuambia acha ushamba mkuu au ndio semina yako ya kwanza
 
Aise umenikumbusha wengine wanabeba pilau minofu ya nyama kwenye mikoba, jamani huko nyumbani hakuna chakula.

Unakuta dada mzuri anatembea nzia nzima ananukia pilau, kumbe kwenye mkoba kafungasha pilau la semina.
Watoto watajuaje kama mama alienda sehemu ina mnuso asipobeba 😅😅
 
hivi nn maana ya TAKE WAY????alaf mleta mada mwenyewe kakimbia angija mniite chap
 
Mi sioni hata tatizo liko wapi ikiwa maji aliyobeba ni share yake.
 
anataka na vipapatio, vidari, sambusa vikatupwe kwenye dustbin na maji yarudishwe dukani
 
Hebu tueleze kwanza..

Kubeba maji ya jero mpaka home.
Ina athari gani?
 
Wewe mwenyewe hukunywa ukabeba ndo mana ukawaona ungekua umekunywa hapo hapo ungebanwa na mkojo ungekua busy kukojoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…