Ni vigumu kuenjoy maisha bila mwanamke, inawezekana lakini ni vigumu

Ni vigumu kuenjoy maisha bila mwanamke, inawezekana lakini ni vigumu

Kaka, ni kweli mwanamke anaweza kuleta furaha, upendo na companionship kwenye maisha, lakini usifanye furaha yako itegemee mwanamke.
Ukijifunza kuwa na furaha ukiwa mwenyewe, mwanamke akija atakuwa nyongeza ya furaha yako, si chanzo pekee cha furaha yako. Jenga maisha yako tafuta pesa, jali afya yako, kuwa na marafiki wazuri, fanya vitu unavyovipenda, jifunze na uwe na malengo.
Usifikiri "nikimpata mwanamke ndiyo nitakuwa complete". Huo mtazamo unaweza kukufanya uvumilie hata mahusiano yasiyokufaa kwa sababu tu unaogopa kuwa peke yako.
Mwanaume mwenye maisha yenye mwelekeo hamtafuti mwanamke ili amwokoe, anatafuta mwenza wa kushirikiana naye maisha aliyokuwa tayari anayajenga.
Kwa hiyo, tafuta mapenzi lakini kwanza jenga uwezo wa kufurahia maisha hata ukiwa single.
 
Back
Top Bottom