Ni vitu Gani huvipendi katika Movie zilizotafsiriwa kwa Kiswahili?

Ni vitu Gani huvipendi katika Movie zilizotafsiriwa kwa Kiswahili?

Mimi zilizofanyiwa dubbing naweza tazama lakini sio za akina DJ mack yani siwezi kabisa.
Movie zilizofanyiwa dubbing kuna vitu uwa wanabadilisha ili mtazamaji aelewi.
Mfano, mtu alisema chakula kitamu kama shushi, lakini mswahili hajui shushi ni chakula gani, so kwenye script wataibadili iwe chakula kitamu kama pilau au kiepe. Au nitakuwa mashuhuri zaidi ya Abdul Kabar, assume ni mtu mashuhuri huko lakini watz hawamjui, basi inakuwa nitakuwa mashuhuri zaidi ya diamond.
Inakera sana hiyo. Au ni ile misemo ya kiingereza inaletwa kwenye kiswahili kama ilivyo hivyo inakosa maana. Mfano msichana anamshauri mwenzie kuwa 'you should play hard to get' wenyewe wanatafsiri ' unatakiwa ucheze mgumu kupata'
 
Sijawahi kujutia kuangalia movie zilizotafasiriwa na Dj mack the mashine kutoka acheche production. Mzuka mwingi kama kawa kama dawa. 😁 Anatafasiri uhalisia uliopo pia anaelewesha vizuri sana. Movie hata kama ni mbovu utaipenda.
Lenie wakishua tujaribu za achecheee 🤣🤣🤣
 
Ukitaka kujua level yakko ya ujinga imefikia kiwango gani anza kuangalia huo upuuzi

Sent from my Redmi 6 Pro using JamiiForums mobile app
Nadhani huna ukomavu wa akili au utakua 20's...ninyi ndo wale limbukeni wa lugha za magharibi wakati mnaungaunga tuu

Kwa macho mapana jamaa wanarahisisha sana kuelewa movie...imagine unaona picha na mtu haelewi lugha ya hiyo movie mathalani wazee nk

Au unafikiri hizo picha zilichezwa kuwalenga ninyi peke yenu mnaojua kingereza cha kwenye ' subtitles' wakati kwenye interview mnatoka jasho?

Futa wrong general perception kwamba kwa sababu watu fulani wanafanya hivi basi wako kama wewe

Bado huyajui maisha...learn to explore it willingly before it takes you there
 
Mimi zilizofanyiwa dubbing naweza tazama lakini sio za akina DJ mack yani siwezi kabisa.
Movie zilizofanyiwa dubbing kuna vitu uwa wanabadilisha ili mtazamaji aelewi.
Mfano, mtu alisema chakula kitamu kama shushi, lakini mswahili hajui shushi ni chakula gani, so kwenye script wataibadili iwe chakula kitamu kama pilau au kiepe. Au nitakuwa mashuhuri zaidi ya Abdul Kabar, assume ni mtu mashuhuri huko lakini watz hawamjui, basi inakuwa nitakuwa mashuhuri zaidi ya diamond.
Safi sana...unayoyasema Dj Mack anajitahidi kiaina
 
Mimi namkubali Dj mjukuu mwana mbambadu japo anauongo mwingi lakini ananogesha muvi kea stori na maneno yako na amefanya niacha hata kuangalia za Subtitle coz hakuna madoido.
😂😂
 
Kuangalia movie usioelewa lugha yake ni Upunguani, Utatoka na nini sasa kama lugha husika huielewi na unakaza fuvu hutaki zilizotafsiliewa si bora ukacheze game tu.
Kana vichwa vina funza kabisa unaanzaje kuangalia movie ya kifaransa,kikorea nk na hizo lugha huzijui tena zinatittle za kigiriki kabisa si kwamba utasoma.
Ni ulimbukeni na kuforce Ughaibu, Vuta chuma iliyotafsiliwa uangalie movie kwa raha sio kwa imagination kama unafunua albam ya Picha mnato(Photo)
Unafuata picha unaelewa
 
Huyu msengerema yaani episode moja yeye anatoa 4. Mnaoangalia hizi series za kutafsriwa mna kazi sana. Episode 1 ina dk 10?
Baada ya bando kupanda, nikasema ngoja nikarushe nilichokutana nacho bora niendelee kudownload tu.
Na matangazo kibao
 
Siku hizi jamaa muhuni sana kuna muvi moja kasema 10 matangazo dk 2 dk 1 anarudia 1 anarudia ya nyuma so muvi inakuwa na dk 7 au 6 .Nilitaka kumpigia simu nimtukane kwa uhuni anaoleta.
 
Naona dj umeamua uingie mzimamzima sababu kitumbua chatiwa mchanga. Dj wa kiswahili ni Afro tu.

1. Anaielewa movie mwanzo mwisho kabla hajaipeleka kwenye hadhira.

2. Ana maneno ya kutia vionjo lakini hakutoi kwenye maudhui ya movie

3. Kiswahili anachotumia kinavutia (lafudhi ya kikenya)

4. Huwapa wahusika majin ya kuchekesha ili mtazamaji asiboeke.

Madj wa bongo hamna kitu
Uzi umevamiwa na Ma dj
 
Siku hizi jamaa muhuni sana kuna muvi moja kasema 10 matangazo dk 2 dk 1 anarudia 1 anarudia ya nyuma so muvi inakuwa na dk 7 au 6 .Nilitaka kumpigia simu nimtukane kwa uhuni anaoleta.
Pole mkuu
 
Inakera sana hiyo. Au ni ile misemo ya kiingereza inaletwa kwenye kiswahili kama ilivyo hivyo inakosa maana. Mfano msichana anamshauri mwenzie kuwa 'you should play hard to get' wenyewe wanatafsiri ' unatakiwa ucheze mgumu kupata'
😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom