Uwekezaji.
Hakuna aliye tayari kuwekeza vilivyo kwenye hii sekta kwasababu soko la filamu kwa hapa ndani (na Afrika Mashariki kwa ujumla) liko tricky sana, hakuna uhakika wa faida kama wenzetu wa wa Asia Ulaya na Marekani ambao wana masoko kwenye nchi na mabara mbalimbali kama China.
Sababu kubwa ya soko kukosa uhakika ni kwamba hakuna njia ya uhakika ya kuuza kazi za filamu na zikafikia watazamaji kwa asilimia angalau 50%, njia ya uhakika kidogo ni CD ambapo wizi wa kazi umeshamiri.
Pamoja na yote hayo, ukweli ambao haufurahishi ni kwamba "kifo cha Kanumba ni pigo kubwa katika safari ya maendeleo ya soko la filamu nchini"... kwanini? Enzi za uhai wake, Kanumba alianza kujaribu kutafuta mwanga kuhusu matatizo yaliyopo hapo juu.
1. Alianza kujaribu kutanua soko la filamu za Bongo kwa kushirikiana na Wanigeria.
2. Steve alikuwa akifanya uwekezaji mkubwa hasa wa fedha kwenye filamu zake.
3. Aliingia mikataba mbalimbali ya uuzaji wa filamu (nasikia).
Jamaa alikuwa masihi wa Bongo movie (my take).
Akitokea mtu akajaribu akaongoza njia katika kutatua angalau baadhi ya matatizo hayo matatu (investment, soko na udhibiti), kutakuwa na exponential efect kwa ukuaji wa Bongo movie.