Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulipiga picha kabisaDah sio powa mwanangu ile nyumba ni nzuri sana ila🙌.
Niliishi Kwa miaka miwili bila shida yoyote ghafla tu mwaka wa tatu nikiwa pale shida zikaanza. Kuna matukio matatu yanilitokea
1.Usiku nimezima taa nilale ghafla naona mtu anapita kwenye Kona ya kitanda anaelekea konani nikajua wenge la usingizi nikapotezea,night nipo kwenye usingizi nasikia sufuria zangu zinafunuliwa mezani ukiwasha tochi au taa hausikii kitu ukizima harakati zinaendelea.
2.Niliamka saa 10 usiku kuoga ili niwahi lindo ile natoka nje nakutana na watu wawili wamekaa katikati ya uwanja tunaangaliana mwili ulisisimka kinoma
3.Nilikuta vitu ambavyo sivielewi vimemwagwa mlangoni kwangu yani kitu kama damu/dawa za kienyeji.
Hili tukio la tatu ndio lilinifanya nisepe kabisa pale na hii ni baada ya kuongea vizuri na wazee wa mtaani na kunipa historia kamili ya ile nyumba Kwa undani.
Na kila mpangaji alikua alikutana na vituko vya aina tofauti tofauti Kuna dada mmoja alikua anakuta kinyesi Cha binadamu katikati ya kitanda.
Hali hii imenifundisha kutafuta taarifa muhimu ya sehemu unayotaka kuamia kabla ya kulipa kodi na kuanza kuishi.
Hiyo picha inaonesha kitu nilichokuta kimemwagwa mlangoni
Hahaha nautajaje mkuu😂😂😂 Na mimi mwanga napaa na ungo ohh.!! Ila huo mpepe unavyoutaja dah!!
Alikufanya nini mzee mwenzangu? Au unipe namba yake ya simu nimuulize yeye mwenyeweMkuu Rehema alinichonifanya sina hamu kabisa na kiumbe yeyote aitwae Mwanamke!
Vipi ulipojitazama hapo kwenye hazina kuu ya taifa hukuona mabadiliko yoyote say uteute mweupe wenye kuteleza? Kama uliona hicho kitu ufanye maombiWenye nyumba wengi wachawi sana!! Kuna siku nimetoka kuoga nikawa napaka mafuta, ghafla nikaona mlango unafunguka wenyewe na nilifunga na funguo.!! Nikatulia nione nani anaingia, holaa hakuna mtu.
Siku nyingine nimelala nimevaa kipensi na tshirt, asubuhi nimejikuta niko kichele 🤣🤣🤣
Nikajua labda itakuwa nimejimix nikaanza kuitafuta ile pensi sijaiona, baada ya siku tatu naona mtoto wa mwenye nyumba ananiletea eti alianua kwenye kamba na nguo zao.!! Nikamwambia hiyo nguo una uhakika umeianua kwenye kamba?? Nikaona anaona km aibu, baada ya siku kadhaa akanisimulia story nzito.
Siku nyingine nimerudi nimechoka nimekaa naangalia tv, naona mkono wa skeleton unanifanyia massage dadeq 🤣🤣🤣🤣
Mwisho nilimtolea uvivu mwenye nyumba akanipa notisi.!! Ila baada ya kuomba mzigo nikamwambia ntamwambia mkeo.
Siji kwako tutakutana Hyatt tu 🙌🙌Nna rafiki yangu akija anapiga simu kabisa tuwafungie mbwa 😂😂😂😂
Waliwahi kumsindikiza kutoka getini mpk ndani, hana hamu nao🤣
Mwenzio nishavuliwa sana mawig mpk siku niliyomzaba ndo alijua wig halitakiwi kutolewa kichwani 🤣🤣🤣
Ila naipenda mimbwa yangu ina uchizi flani naenjoy sana.!! Kuna mwanaume alikuwa anajifanya jeuri alikuja kwangu nikamsakizia acheze nao, mpaka leo ananimind 🤣🤣🤣
Ili shawai kunikuta kama ivi Ila kalikuwa na miaka 12 baba yake alikuwa mjeshi pale Ihumwa Dodoma. Nika msanua kwa baba yake. Baba yake kwa Asira akampeleka kwa bibi yake kijijini nikabaki salamaNyumba nyingine nilihama sababu ya mtoto wa mwenye nyumba. Ni mdogo 13 years ananiambia uncle nakupenda nataka uwe my boyfriend. Si unajua hivi vitoto vya English Medium.
Nikaona hapa siku sio nyingi nitaitwa mbakaji. Katoto kuna siku kamekuja ghetto, kanajichekesha chekesha tu, nikakauliza Jacqueline how can I help you? Kakajibu nothing, just close the with a key, I want to sleep with you.
Aisee akili ikaniruka nikasema huyu Mzee wa Kichagga kamtuma mwanawe ili nitolewe kafara?
Kimbembe ikawa namna ya kukaondoa chumbani bila ya kukatimizia ndoto yake.
Nikakapa 10,000 nikakaambia kakalete soda baridi sana tuwe tunakunywa kabla hatujalala.
Kalipotoka, nikafunga mlango nikaondoka nikaanza kurudi usiku mkali,.Hadi nilipopata nyumba ya kuhamia
Duh pole sana mama,nimesikitishwa mno na hilo,ikikupendeza nicheki pm unitumie namba yako ya wasap tuliongelee hilo nikutumie pesa ya kununua vyupi vingineNa nyumba nyingi dar ndio mchezo wao dadekii unakosa hata pesa ya kunukua vyupi 😁😁😁
Huko nimepita mkuu ni zamani kwa sasa nashukuru niko njema.Duh pole sana mama,nimesikitishwa mno na hilo,ikikupendeza nicheki pm unitumie namba yako ya wasap tuliongelee hilo nikutumie pesa ya kununua vyupi vingine
Njoo bff ntawafungia bana 😂😂😂Siji kwako tutakutana Hyatt tu 🙌🙌
Umenena kwa lughaMxiieeeeewww!! Muda wote mnawaza ujinga tyuu.!! Mapombuo yako!!
😂 dah ni kipengele mkuuUngefunga saba kavu
Aisee.Nakumbuka miaka hiyo ndio nimepata kazi benki Fulani, nikapata nyumba Sinza ya mama mtu mzima kijana.
Akanikaribisha sana, hakuwa na noma, nilipokuja kununua flat TV enzi hizo plasma tv ndio zimetoka, hamna cha LCD na LED ni ndoto kabisa, yaani ndio kwanza watu wachache sana tumeamza kujikwamua kutoka kwenye machogo.
Basi yule mama akawa anataka muda wote aje ashinde ghetto kwangu, anavaa nguo very light.
Kuna siku jumamosi nimemaliza kufua, nikasema Leo nijilipie, nikachukua Konyagi kubwa, nikawa na Dodoma wine, kwenye oven kilo mbili za kitimoto zinaokwa taratibu. Mara ghafla mlango unagongwa huku mtu akiingia ndani bila kukaribishwa.
Nilikuwa Niko na boksa tu sikuwa natarajia mgeni, akaniudhi sana. Nikakimbilia taulo, akanifuata akanivua taulo. Nikasimama wima hasira Imenijaa.
Akaanza kujiliza ohh Mimi nakupenda siku zote, wewe unajidai huoni.
Nikamkaripia nikamwambia anikome. Baada ya hapo alianza chuki na visa, nilikaa miezi minne tu nikahama.
AiseeMimi na wasela wenzangu enzi hizo tuko form six, katika kujiandaa tukaona ni vyema tupange chumba ili tuweke Kambi ya masomo.
Usiku mmoja nikashtuka usingizini, tukamuona baba mwenye nyumba na mkewe na watoto wako uchi wa mnyama wanaizunguka nyumba.
Nikawaamsha wenzangu. Chumbani kuna Giza hatujawasha taa hivyo tunawaona kwa uzuri sana.
Baada ya wiki tu tukahama. Walikuwa Wana roho nzuri sana utadhani watu kumbe ni mashetani
Kwa hiyo ndiyo ukamchukia huyo "mama mtu mzima kijana"?Nakumbuka miaka hiyo ndio nimepata kazi benki Fulani, nikapata nyumba Sinza ya mama mtu mzima kijana.
Akanikaribisha sana, hakuwa na noma, nilipokuja kununua flat TV enzi hizo plasma tv ndio zimetoka, hamna cha LCD na LED ni ndoto kabisa, yaani ndio kwanza watu wachache sana tumeamza kujikwamua kutoka kwenye machogo.
Basi yule mama akawa anataka muda wote aje ashinde ghetto kwangu, anavaa nguo very light.
Kuna siku jumamosi nimemaliza kufua, nikasema Leo nijilipie, nikachukua Konyagi kubwa, nikawa na Dodoma wine, kwenye oven kilo mbili za kitimoto zinaokwa taratibu. Mara ghafla mlango unagongwa huku mtu akiingia ndani bila kukaribishwa.
Nilikuwa Niko na boksa tu sikuwa natarajia mgeni, akaniudhi sana. Nikakimbilia taulo, akanifuata akanivua taulo. Nikasimama wima hasira Imenijaa.
Akaanza kujiliza ohh Mimi nakupenda siku zote, wewe unajidai huoni.
Nikamkaripia nikamwambia anikome. Baada ya hapo alianza chuki na visa, nilikaa miezi minne tu nikahama.
ChaiMwenye nyumba alikuwa na shida sana ya pesa.
Kila wakati vibom.......
Nikatamani kuhama nikaona sio issue
Nikamwambia aniuzie nyumba akakubali
Yeye akageuka kuwa mpangaji wangu
Ila nilikuwa sichukui kodi kwake