Ni vituko gani ulishawahi kufanyiwa na mwenye nyumba wako hadi ukatamani uhame uache Kodi?

Walikuwa wanaweka zindiko la kuzuia wachawi, ungeangalia vizuri ungemuona mganga
 
Aah sasa we ukutane na mama mwenye nyumba yuko msela poa tu si mnakula mipango.
Hela ya msosi ipo kwake mi bachelar tu miaka hiyo,
Ye mwenyewe sa ingine anakula microfone check.
Yaani pale hata mke nilikua sitaki.
Lunch naletewa mapema tu
Usiku narudi nshakula ,namtoa ya siku nalala.
Maskini mama wa watu
Simjui nilipanga tu.
Mama anakuuliza Baba leo utakula nini?
Ninachotaja mchana sinia hili hapa.
atahakikisha kakaa pale pembeni mpk nile nishibe.
Namkumbuka sana huyu mama maskini.
Hatujaonana tena miaka mingi sana
 
Nyumba za kupanga zina vimbwanga sana. Sitazungumzia zote ila za kusisimua tu.

#1. Mwenye nyumba alikuwa mjane wa kichaga. Complainer anakaa on the other side of the road. Kiufupi nilipanga chumba 4 months ila sikuishi pale nikawa nalala kwa manzi yangu. Kuna siku mwanangu mmoja kaja kwa ajili ya kuvaa joho nikampa key akalale pale maana palikuwa free tu. Maza kusikia hilo alikuja kunidai hela eti sababu jamaa alitumia choo na bafu lake kwa siku tatu alizokaa. Nililipa buku 20 ila mkataba ulipoisha tu nikaendelea kulipa kule alikokuwa manz yangu. Napo tabu ilianza maana mama mwenye nyumba alikuwa mdada nesi flani ila akawa ananichukia toka siku nimetambulishwa kwake. Baadae vikaanza vituko mjengoni mabati kulia lia usiku ndoto za ajabu nikahamaga pale.

#2. Nilipanga fully fledged apartment kwa ajili ya kuanza practice ya kuishi kifamilia. Ile nyumba ilikuwa ni mpya kabisa hajawahi ingia mtu ziko nyumba kama 7 kwenye compound ya Don mmoja. Nyumba ilikuwa kali sana yani ila tatizo likaja a few month later. Nilikuwa napata misisimko ya mwili na nywele hivi ukikaa sebleni kwenye kochi unaskia sauti kama za mvumo wa upepo. Kama ushaangalia movie za kinaijeria scene za kichawi kuna sauti flani wanawekaga ile. Saa zingine unahisi kama watu wanatembea hivi unaskia vishindo tu na kuona vivuli vinapita. Nilikuwa naishi na manzi yangu ila ni kipindi ambacho tulikuwa na ugomvi usioelezeka. Mnaweza toka mihangaikoni freshi tu ila mkifika tu pale ndani ugomvi unapotokea hata haijulikani, yani alikuwa na visirani vya hatari. Niliishi pale miezi 10 maji yalipozidi unga nilidai kodi yangu ya miezi miwili iliobaki nikahama na ule mkoa kabisa.

#3 Nilianza life upya bongo baada ya upepo wa Covid kuniramba nikajiegesha Migomigo kwenye kibanda kimoja cha urithi wa watoto flani wa kizaramo. Balaa likaja kodi inagombaniwa kama mpira wa kona. Baba yao alizaa na wake tofauti hivyo kila mtoto akajiona ana haki na mama yake wale kodi. Waligawana vyumba wakawa wanagawana kodi tuπŸ˜‚ mara wazurumiane kesi zikawa haziishi kwa mjumbe. Majirani nao watu wa kushinda vibarazani ni husda, umbeya na uzandiki ondoka usemwe. Mbaya zaidi nilikuwa nimepaki mkweche wangu mbele ya nyumba basi ile tofauti ya lifestyle ikawa naonekana naringa kisa nina chombo uwani na naenda kazini daily na kurudi jioni. Umeme nao ulikuwa uduwanzi staki hata kuelezea. Nikaseti mipango ya kuvuta "stove" ilipokamilika tu nikahama kabisa pale.

#4. Kero hazikosekani ila walahu siishi na waswahili tena😁 na mipango ni kuwa nikitoka hapa nihamie kwangu kabisa. Mstaafu anasumbuaga mapema kabla ya muda wa kodi kufika ila namlipa in advance ili mimi niwe namdai miezi ndio imekuwa solution. Nimegundua pia mkewe ni mbegu ya kikwere hujifanyaga social sana ila ana ki jealous cha kipuuzi kila nikifanya mambo ya maendeleo nimekata mazoea nao sahizi.
 
Kwahiyo unampiga kende Landlord wako
 
Duh unaamka asubuhi unakuta umevuliwa kipensi!!! Hapo kama ulikuwa hujanyoa nahisi ulijisikia aibu sana baada ya jamaa aliyekuvua kipensi usiku kuona hazina kuu ya Taifa ina nywele kama zote
 
Wakati wa Tendo takatifu anakuja kudai kodi kwa mume wangu, kipindi tukiwa vijana Pale kinondoni Moscow.
 
Unemla sana aisee
 
Unemla sana aisee
Sijawai aisee,ila nilikua naenjoy sana nikiwa nae.
Ni mmaza alikua ananijali sana na hanifuatilii.
Kazi zangu usiku
Nikirudi asubuhi kaniwekea vitumbua na chai ya maziwa.
Nikiuliza mchana vp.
Ananipa bajeti nzima.
Haizidi 10,000.
Sa ingine ananipa buku tano kupunguza gharama namwambia kausha tu.
Familia yake ilikua kubwa sana,mitoto mivibaka
Inazaa inamletea watoto na yenyewe yanakaa humohumo.
So nafkiri mmaza alikua anakuja gheto kutuliza moto tu
Hatukuwai kunyanduana,ila mapenzi km yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…