Ni wakati muafaka sasa Mbowe kuachana na mikutano ya Rais Samia

Nimemdharau sn huyu maza
 
hatari sn
 

"Kinachofanywa na Rais kwa sasa ni kuonyesha unafiki wake kuwa ana nia njema ili serikali yake iendelee kupata uungwaji mkono na kupata misaada ya kimataifa katika kuiendesha."

Kauli ya kitumwa kabisa kabisa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anapaswa kufanya kile kilicho sahihi kwa watanzania na kinachoungwa mkono na watanzania. Kwamba anafanya vitu ili aungwe mkono sijui na nani kutoka nje nafikiri ni mawazo ya wapinzani pinzani ambao upinzania wao, na pengine uanzilishi wa vyama vyao ulilenga kukidhi matakwa ya hao watu wa nje. Ndo maana pengine hata siasa za hao wanasiasa ni za performance tu, kuigiza tu kwamba mpo kwenye ushindani wa kisiasa but kimsingi ni kutetea maslahi binafsi. Mtachelewa sana kuelewa watanzania wanataka nini.
 
Wajinga nyie, chama tawala hakina ulazima wa kukutana na Cha upinzani, ni Siasa za kistaarabu za Samia tu
 
Kwa nini Samia akienda kumtembelea Mbowe haitangazwi
 
Huu siyo ushauri Bora kwa Mh Freeman Mbowe.

Hiyo hapo ni game iko kwa uwanja...

Game inachezwa na siyo kukaa pembeni na kulalamika au kususia mikutano ya Maendeleo kisiasa!!
 
Tatizo usipokwenda watasema tuliwaita kwenye mazungumzo halafu hawakuja, kelele zitaanzia hapo.

Ili kuwafunga midomo hawa ni dawa yao ni kwenda, halafu uone kama kweli wana nia na kile wanachosema, kuwa na subira kidogo ili uzione nia zao.

Wakionekana hawako tayari kama wanavyofanya sasa ndio kujiondoa, hapa utapata la kuwaambia watanzania, na wao watakuwa wameuona ukweli, then waachie aibu yao hao matapeli.
 
Kwa sera hizi za kuomba omba misaada ili Samia aweze kufanikiwa sharti asimamie utawala wa sheria. Kama na hili hufahamu basi utakuwa chawa!
 
Dogs Covid-19. Sad for Mr. Mbowe.
 
Changamoto ndio zilezile tu hata yule jamaa alizikuta na kaziacha kama hivi zikiendelea hakuna jipya.
 
Kesi imefunguliwa na civid-19 mawakili wa serikali wanaingiaje kuwatetea?
 
Kwa sera hizi za kuomba omba misaada ili Samia aweze kufanikiwa sharti asimamie utawala wa sheria. Kama na hili hufahamu basi utakuwa chawa!
Ukinifuatilia utagundua kuwa mimi siyo fan wa falsafa ya Samia. Simchukii yeye binafsi kama mama au kama mtu ila sipendi mambo yake ya ukikwete, ya kuiendesha nchi kiutegemezi na kiuwakala.

Afu bado unazidi kudhihirisha mentality za kitumwa tumwa tu. Hivi kuna sifa gani katika kupata misaada kana kwamba kiongozi wa nchi kama alivyo Samia inambidi au inampasa aonekane kufuata misingi ya sheria za nchi yetu? Hivi Samia anawajibika kwa wanaompa msaada au anawajibika kwa wapiga kura wake? Embu jipe muda uone ubovu wa fikra hizo: atakuwa rais wa ajabu sana kusimama mbele za watu na kujitapa kwamba amefanikiwa kukusanya misaada huku na kule kwa sababu amefanikiwa kusimamia utawala wa sheria. Ni kujaribu kusema kwamba Tanzania si nchi huru na kwamba usimamizi wa sheria zetu ni kwa ajili ya kuwafurahisha watu wengine zaidi ya watanzania.
 
Ingekuwa vema sana kama hayo maswali yako kuntu kabisa ungeyaelekeza kwa Samia mwenyewe kwa kuwa ni yeye anayejitapa na kushangilia kufanikiwa kupata mikopo!

Mawazo ya kitumwa anayo yeye kwa kupenda pesa bila jasho! Nadhani hii ni tabia ya wanawake wengi!
 
Wajinga nyie, chama tawala hakina ulazima wa kukutana na Cha upinzani, ni Siasa za kistaarabu za Samia tu
Tuendelee na ubabe Kama wa Magufuli aliyeiba uchaguzi kishamba Hadi akasahau kuwa wabunge wa upinzani Ni muhimu kwa masirahi ya serikali
 
CDM kwa sasa hawana ajenda
 
Sawasawa. Na hata hiyo dhana inayojengeka kwamba ule unaoonekana kama "usoft" wa Samia kwa wanasiasa wa upinzani ni facade ya kuwadanganyia kule anakoomba misaada lazima ikustue ukiwa mtanzania wa kawaida. Sidhani kama ni afya, si kwa upinzani na si kwa Samia mwenyewe, kujenga taswira kwamba uhusiano wa vyama vya siasa nchini unajengwa kwa misingi ya ili kukubalika ugenini. Vyama vya siasa vinawajibika ( au vinapaswa kuwajibika) kwa watanzania na watanzania peke yake. Haviwajibiki kwa mreno, wala mjerumani wala kwa mwarabu au kwa watu gani huko wa sayari fulani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…