Ni wakati muafaka sasa Mbowe kuachana na mikutano ya Rais Samia

Ni wakati muafaka sasa Mbowe kuachana na mikutano ya Rais Samia

Sawasawa. Na hata hiyo dhana inayojengeka kwamba ule unaoonekana kama "usoft" wa Samia kwa wanasiasa wa upinzani ni facade ya kuwadanganyia kule anakoomba misaada lazima ikustue ukiwa mtanzania wa kawaida. Sidhani kama ni afya, si kwa upinzani na si kwa Samia mwenyewe, kujenga taswira kwamba uhusiano wa vyama vya siasa nchini umejengwa kwa misingi ya ili kukubalika ugenini. Vyama vya siasa vinawajibika ( au vinapaswa kuwajibika) kwa watanzania na watanzania peke yake. Haviwajibiki kwa mreno, wala mjerumani wala kwa mwarabu au kwa watu gani huko wa sayari fulani....
Kuwajibika kwa wananchi sawa lakini kutokubalika kimataifa ni tatizo kubwa kisiasa na kiuchumi!
 
Bunge lipo huru jamani"mama" hausiki na maamuzi ya spika😆
 
Mkuu, ni haki yako kutoa haya maoni, lakini hapa hujamtendea Mbowe na Mazaa haki! Haya mambo yanataka muda, pia mchakato wa kisheria unaoendelea ni sahihi! Wote tukubaliane kwamba alicho fanya Ndugai
Kwa wale wabunge 8 wa CUF, kilikua ubakagi wa demokrasia! Kwanini Civid-19 wafanyiwe vile vile?!
Lakini pia, kama maamuzi yakiwa yale, alafu tuanze kuitwa ccm b, tutajiteteaje? Wacha Kibatala na team yake wapige kazi, siyo kupewa ushindi wa mezani!
 
Kuwajibika kwa wananchi sawa lakini kutokubalika kimataifa ni tatizo kubwa kisiasa na kiuchumi!
Kwani mataifa yapo mangapi duniani? Uhusiano wa taifa na taifa haupaswi kujengwa kwa misingi ya mahusiano yenu ya ndani ya taifa. Ukiona taifa linatulazimisha tuwe na mahusiano baina yetu ya namna fulani huo hauwezi kuwa uhusiano wa mataifa wenye afya.
 
Kiini cha tatizo ni Joyce Mukya. Mbowe angechomoa Covid mmoja amweke huyo hawara wake ili hili suala liishe. Covid19 wakae kikao na kukubaliana kuachia nafasi moja kwa ajili ya Joyce Mukya hawara wa mwenyekiti.
 
Kwa uamuzi huu wa Spika kuhusu kuendelea kwa Halima na wenzake 18 kuwa wabunge ni dhahiri dhahiri Samia na serikali yake hawaheshimu kabisa katiba iliyopo. Tumeshudia na kusikia Jaji Mkuu Prof. Juma akiamuru mahakama kutopingana na serikali vilevile tumemsikia Spika wa Bunge akisisitiza utiifu wake hoja zote za serikali, hivyo tusitegemee hata mara moja vyombo hivi viwili vya dola kutenda haki pindi serikali inapovunja katiba na sheria.

Bunge na Mahakama kwa sasa ni vyombo vya serikali kwa manufaa ya serikali. Hakuna tena mihimili mitatu ya dola bali kuna muhimili mmoja wa serikali.

Kwa hiyo nashauri Mbowe kuachana kabisa na mazungumzo na Samia na serikali yake kwa sababu hakuna kitakachoafikiwa kutekelezwa. Kinachofanywa na Rais kwa sasa ni kuonyesha unafiki wake kuwa ana nia njema ili serikali yake iendelee kupata uungwaji mkono na kupata misaada ya kimataifa katika kuiendesha. Mbowe atambue kwamba hata kufutiwa kwake mashtaka ya ugaidi ni mbinu ya Samia kujikosha mbele ya mataifa ya kigeni.

Samia anapenda sana kutalii nje ya nchi hivyo ili kupunguza kelele za madai ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba mpya awapo kwenye utalii wake ambapo amepanga kutembelea nchi nyingi, kete yake kubwa ilikuwa kumwachia huru Mbowe.

Serikali ya Samia bado inaendeleza udikteta na kamwe haitaacha sera za ukandamizaji za mtangulizi wake Dikteta Magufuli!
Nakazia
 
Samia anapenda sana kutalii nje ya nchi hivyo ili kupunguza kelele za madai ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba mpya awapo kwenye utalii wake ambapo amepanga kutembelea nchi nyingi, kete yake kubwa
Kama hilo ndio lilikuwa lengo la kumuachia Mbowe, basi amefanikiwa.
 
Kama hilo ndio lilikuwa lengo la kumuachia Mbowe, basi amefanikiwa.
Ndiyo hilo kwa kuwa bila hivyo angekuwa na kigugumizi kwenda nchi ambazo angekutana na mabango ya "Mbowe is not a terrorist" "Mbowe siyo gaidi"
 
Back
Top Bottom