Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mayala, sijui nitumie neno gani, maana nisijekutafsiriwa vibaya, ilihali heshima yangu kwako haijawahi kukosekana.Japo ni kweli lakini sio busara kufanya ukosoaji kwa kutumia maneno makali yenye lugha ya maudhi, wewe huna Ph.D, ripoti ya Ph.D holder, huwezi kuita "a professional rubish". Hata akina sisi tuliikosoa ripoti hiyo lakini tulitumia lugha ya kistaarabu! Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni swali tu...
Serikali, mabenki na taasisi za fedha ziko huru kusamehe sehemu ya deni au deni lote, kitu muhimu ni wenye fedha zao kujulishwa. Licha ya umasikini wote uliotopea wa nchi yetu, hakuna ubaya wowote kusamehe deni lolote kwa yeyote, lakini lazima utoe sababu why unasamehe, ila pia unaposamehe majizi ndio muhimu zaidi kuwa transparent, ili isije kuonekana viongozi wetu wamekuwa compromised !.
Kwenye hili aombwe radhi kwa lipi?.
P
Kwa ufupi kabisa, niseme tu kuwa, utumie akili na maarifa yako vizuri. Kujifanya mjinga wakati una akili ni kudhihaki kazi ya muumba wetu aliyetujalia ufahamu.
Hakukuwa na deni la trilioni 360, hivyo hakukuwepo na msamaha. Hakuna tulichosamehe, bali tuliomba tupewe chochote, tukakubaliwa kupewa $300m ndani ya kipindi cha miaka 7, na hizo pesa zitakuwa zinatoka kwenye mauzo ya makinikia. Installment ya kwanza itakuwa baada ya kuruhusu makinikia yaliyozuliwa, yasafirishwe. Tukatii amri. Halafu tukasaini makubaliano kuwa, kwa vyovyote iwavyo, siku za mbeleni, hata kukiwa na mgogoro, kamwe hatutazuia usafirishaji wa dhahabu wala makinikia, tutaenda kwenye meza ya mazungumzo. Suluhisho lazima liwe limepatikana ndani ya siku 30. Ikishindikana, mahakama ya biashara ya Singapore itaingilia kati na kutoa maamuzi, na maamuzi yake hayatakatiwa rufaa mahali popote na upande wowote.
Hatukuwa na madai, hatukutoa msamaha kwa sababu hakukuwa na chochote tunachokidai, tulipewa pesa ya msaada, kama tunavyosaidiwa na mataifa wahisani.